Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
Banana Zorro PDF Print E-mail
19 Oktoba 2010

Banana Zorro ni mmoja wa wanamuziki wa mwanzo kabisa katika uwanja wa Bongo Flava au Muziki wa Kizazi Kipya. Banana ni mtoto wa mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki Tanzania, Mzee Ally Zorro.

Banana aliingia kwenye gemu na singo za "Anakudanganya" na "Big Boss", halafu akaunda kundi na mwenzake aliyekuwa anakwenda kwa jina la Masiga, kundi lilikuwa likijulikana kama "B love M"

Mwaka 2002, Banana akaachia albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Banana", mwaka 2006 ikafatiwa na "Subira". Jamaa anasifika kama mwanamuziki 'kiraka', anachafua engo zote za muziki wa kizazi kipya, toka kwenye rhumba, mwanamuziki wa kujitegemea hadi muziki wa bendi. Utakumbuka kwamba Banana amewahi kufanya muziki na bendi kubwa ya InAfrika. Banana pia ameshirikiana na wanmuziki wengi sana kama Bushoke na Soul n Faith.

Baadhi ya nyimbo zake zilizowahi kubamba vilivyo ni Nimekuchagua Wewe, Mama Yangu, HaoHao, Nataka Niwe Nawe, Sinyota, Safari, Ninakuona, Mapenzi ya Simu, Jua Linazama, Wangu Maria, Mama Kumbena, Zoba, na zingine nyingi.

Mwaka 2010 alifanikiwa kushiriki katika tamasha kubwa kabisa la muziki katika Bara la Afrika, tamasha la Sauti za Busara.

 

 

Maoni  

 
+15 #9 rich joel 2011-02-14 14:40
daaaaaaaaaaaaaa a we ni noma broooooooooo haufunikiki da wni soooooooooooooo
 
 
+3 #8 Godfret ntarani 2011-01-23 14:34
Safi sana Kaka mkubwa pamoja jina kubwa ulilonalo lkn bado umeukontrol umaarufu ongela sana niwachache mno like u guy.
 
 
+3 #7 p bang 2010-12-29 18:37
ebwana your more than a normal musician since da song mama to nzera and others anyway may be its all about mtoto wa nyoka ni nyoka' keep it up. but we need to see you with internationalmu sician make our country proud by going beyond our nation man you can politician have failed but you musician can do something
 
 
+3 #6 Neema 2010-12-07 09:35
Uko juu mkubwa
 
 
+2 #5 Betty 2010-11-25 11:16
Yaani kati ya watu ambao hawabahatishi katika fani, basi wewe ni ICON!!!!!!
 
 
+2 #4 kishe 2010-11-22 08:41
banana unatisha, nakukubali kwakua huchuji kla kukicha upojuu kazabuti
 
 
0 #3 bonge haule 2010-11-15 14:05
Big up Banana unakubalika katika kila rika! Big uuuuuuuuuuuuuuu uup!
 
 
0 #2 chumuu 2010-11-13 16:32
banana anatishaaaaaaaa aaaaaaa, thats all i can say..
 
 
0 #1 Nancy 2010-11-06 12:44
Ki ukweli Banana uko juu sana kaza buti Mungu atakusaidia.
 

Weka Maoni

Security code
Upya

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.