Wiki hii, msanii wetu wa wiki ni binti Nuru Magram. Ingawa hatujamsikia kwa muda mrefu, vibao vyake huwa vimesimama kwelikweli.
Nuru aliingia katika gemu miaka ya 2000 ya mwanzo, na akatoka na kibao cha kwanza kiitwacho "Walimwengu".
Kisha akakifuata hicho kibao na ngoma ya "Msela" ambayo video yake imetulia mno. Na baada ya "Msela", alitoka na kibao cha tatu kiitwacho "Kwanini".
Kwa sasa, Nuru ana mkataba na studio ya Soul House Vibes, mjini Stockholm, Sweden ambako ndiko anakoishi tangu mwaka 1990. Wasanii ambao Nuru anasema angependa sana kushirikiana nao ni pamoja na Enika, Mwasiti, Chid Benz na Professor Jay. Enjoy Nuru, Msanii Wetu wa Wiki - kamata kitu hiki hapa:
|
Maoni
RSS