Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
Ramani

Historia
Kalumbi na Makatani ni miji ambayo ina hazina kubwa ya historia ya kiafrika. Ni katika miji hii watumwa toka katikati ya Afrika walipitishwa wakielekea pwani kwenda kuuzwa kwenye mabara mengine. Baadhi ya watumwa hao walibakishwa katika miji hii miwili kama vibarua katika mashamba ya mkonge.

Kalumbi Map

 

KALUMBI
Mji huu uko juu mlimani ukipakana na mji wa Makatani ambao uko bondeni, miji hii miwili inatenganishwa na barabara ya vumbi yenye umbali wa kilomita zipatazo kumi na mbili inayokatiza katika bonde la ufa. Mvua zinaponyesha kwa wingi mara nyingi barabara hii huharibika na kupoteza mawasiliano kwa miji hii miwili, kwa muda mrefu wakati mwingine.

ImaKutokana na hali nzuri ya hewa katika milima ya Kalumbi wakoloni waliamua kuufanya mji huo kuwa makao makuu yao japo kuwa mji wa Makatani ulikuwa mji mkubwa wa kibiashara, ulio karibu na barabara kuu ya taifa pamoja na reli.
Kitega uchumi kikubwa katika Kalumbi ni utalii, kuna mahoteli makubwa na sehemu za kupiga kambi ambazo ni vivutio vikubwa sana kwa watalii wa kigeni.

Kaskazini Kalumbi inapakana na miamba mikubwa inayosemekana kuwa na madini ya thamani ikiwamo dhahabu. Huku ndiko anakoishi babu yake Man Carlos. Ni miaka ya hivi karibuni tu ndio vijana wa hapa wameanza kufahamu umuhimu na thamani ya madini yaliyo katika milima hii.

PeterUpande wa magharibi wa Kalumbi kuna misitu ambayo imeanza kuvunwa kwa ili kupisha shughuli za kilimo. Kahawa, matunda na mbogamboga zinastawi sana katika udongo wa mahali hapa.
Nje kidogo ya mji huu ndiko wanabendi wa Homeboys wanakoishi pamoja na familia zao na marafiki zao. Ray, Imani na Peter wamekulia katika mtaa wa Kijiwe.

Kalumbi ina taa moja tu ya kuongozea magari, katika makitano ya barabara ya Julius Nyerere na ile ya mtaa wa Samora Machel. Barabara zote zimesheheni majengo ya kikoloni ambazo ni ofisi za Wilaya, hoteli ya nyota mbili, pamoja na maduka kadhaa. Moja ya majengo mojawapo imegeuzwa kuwa jumba la kupangasha linalojulikana kama Jasmine Arcade, biashara kadhaa zimepanga hapa.

Kuna msikiti wa zamani sana karibu na kituo cha daladala, mbele kidogo ya mnara wa saa.

Pia kuna hospitali ya zamani ya wamishionari wa Kijerumani pamoja na shule ya sekondari karibu na mwisho wa barabara ya ya Julius Nyerere.

MAKATANI
Tofauti na mji wa Kalumbi, udongo wa haba hauna rutuba ya kutosha kutokana na shughuli za kilimo cha mkonge kilichofanyika mahala hapa kwa muda wa zaidi ya miaka 100.
Hali ya hewa ya hapa ni ya joto na vumbi jingi. Ni mji uliochangamka kibiashara hasa katika makutano ya barabara mbili za kitaifa pamoja na reli ya kaskazini-kusini.

Kituo cha treni cha hapa ni kikubwa kuliko mahitaji yake, kuna mabehewa yaliyochakaa sana karibu na shamba/kiwanda kubwa la mkonge, yanaonekana kutelekezwa.

Kuna vibanda vya wachoraji wa picha za tingatinga katika makutano ya barabara hizi mbili za kitaifa. Vibanda hivi na kazi zake za tingatinga ni kivutio kikubwa cha kitalii kwa watalii wanaotoka katika fukwe za bahari za mashariki pamoja na mbuga za Serngeti.

Pamoja na kuwa ni mji mkubwa wa kibiashara, Makatani ina majengo mchache sana ya kuvutia ambayo inaweza kujivunia nayo. Mahala hapa mfumo wa uzalishaji mali usio rasmi ndio hasa uliojikita.

Sehemu muhimu katika mji huu ni kilabu cha Le Mafichoni, Kilabu cha Mkonge cha Makatani, pamoja na Radio Masifa Fm.

 

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.