Amini ni mmoja wa wasanii waliopata umaarufu kwa haraka sana katika muziki wa Bongo Flava au muziki wa Kizazi kipya kama unavyofahamika.
Jamaa alianza kazi yake ya kuimba akiwa na mkali mwingine wa THT, Baranaba, na jamaa hawa wawili wamekuwa kila nyimbo wanayoipeleka hewani wanahakikisha inabamba.
Nimejaribu kujiuliza iwapo Amini ni msimulizi mzur iwa visa kwenye nyimbo zake, nikakubaliana na nafsi yangu kwamba nimepigia jawabu mstari. Nimeiangalia video yake ya Robo Saa kwa kitambo kirefu tangu itoke, na kwa kweli Amini ni mtu mwenye kipaji cha kipekee na mwenye maono yanayofurahisha roho pale unapotazama kazi zake. Unapata kile ambacho amekusudia.
Hebu wiki hili tueselebuke kidogo na "Bado Robo Saa."
|
Maoni
KWANI ALIVYO KIJA ALIJIPANGA VILIVYO
AMINI WE LOVE YOU
GOd Bless youuuuuuuuuuuuu uuuuu!
RSS