images/stories/news_flash/kiba.jpg Wengi wetu tunamfahamu kama "Msinderella", kwani "Sinderela" ndo ilikuwa ngoma yake ya awali ambayo ilimchora kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya. Akafanya shoo kadhaa na kurekodi nyimbo
kadhaa, nabii akapendwa nyumbani.
Muda si muda tukasikia msela yuko ughaibuni, UK, tukadhani labda kenda mara moja halafu atarudi, mara tukawa tukisoma tu kwenye vyombo vya habari kwamba jamaa oda za kupiga shoo huko zinaongezeka. Wenye akili tukajua, Ali Kiba si mwenzetu tena, nyota yake tayari imeng'aa.
Hivi majuzi tukasikia tena kaitwa katika mradi wa muziki wa ONE8, mara ghafla tukasikia audio na video, kwenye video jamaa akawa kazungukwa na wakali kibao toka nchi za Kiafrika, ila kubwa zaidi ni ile kupiga saundi na video chini ya usimamizi mkali wa mfalme wa R&B duniani, R. Kelly. Kikubwa ni kwamba Kiba amepeperusha si tu bendera ya Tanzania, bali pia kiswahili katika mradi huu.
Hongera sana Kiba, na wewe ndo mkali wetu kwa juma hili. |
Maoni
RSS