Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?

Je kuna msanii unayemfahamu na hayuko kwenye wavuti yetu? BOFYA HAPA KUMUWEKA

Wagosi wa Kaya

Hili nikundi lenye makao yake mjini Tanga na linajumuisha wasanii wawili Frederick Mariki ama Mkoloni na John Simba

ama Dr John. Wagosi wa Kaya inatokana na lugha ya kisambaa lenye maana ya watoto wa nyumbani. Walijiunga pamoja mwaka 1996 na walianza kufanya maonyesho katika matamasha mkoani tanga na baadae umaarufuwao uliongezeka haraka na kujulikana nchini kote. Muziki wao ni wa kipekee ukipigwa kwa mtindo wa bongo fleva.

 

Wagosi wa Kaya walikonga nyoyo za mashabiki wao ambao wengi wao ni masikini kwa kuwa nyimbo zao zina mvuto na namna ambavyo wanaziimba. Nyimbo zao zinagusa matatizo yanayowapata wananchi wa kawaida kama hali ya hospitali, rushwa ndani ya jeshi la polisi na maeneo mengine kama kutofanya vyema kwa timu ya soka ya taifa.

Wimbo wao wa Tanga Kunani ulipigwa marufuku na mkuu wa mkoa akidai kuwa unadhalilisha mkoa wake. Kundi hili linawakilisha ubunifu wa kimuziki wa hiphop yenye mahadhi ya Kiswahili huku wakiimba katika namna ambayo ni ya kuchekesha na lafudhi yamakabila ya mkoa wa Tanga.

 

Kundi hili limekwisha toa albamu tatu, Ukweli Mtupu (2001), Ripoti Kamili (2003) na Nyeti (2005). Wagosi wa Kaya ni mojawapo vikundi asilia vya bongo fleva na ambavyo ni lazima viwepo ktk matamasha ya muziki wa Kiswahili.

 

Maoni  

 
0 #6 uniawupihuc 2019-11-13 23:02
http://mewkid.net/where-is-xena/ - Buy Amoxicillin Online Amoxicillin No Prescription gmg.many.wahapahapa.com.dnv.yk http://mewkid.net/where-is-xena/
 
 
0 #5 aphirqum 2019-11-13 22:45
http://mewkid.net/where-is-xena/ - Amoxicillin Amoxicillin No Prescription dnu.jmqp.wahapahapa.com.rdw.lz http://mewkid.net/where-is-xena/
 
 
+5 #4 warudi tena bana 2011-03-21 20:03
siku hizi watoto wanimba ujinga tu bora hawa jamaa warudi ili jamii itoke gizani wanafichua kweli uovu na wizi kwa viongozi wetu bila uoga wala kufichaficha..ni wajasiri je profesa j na wengineo mnaweza huu moto nyie ccm?
 
 
0 #3 pipi 2011-01-22 23:37
jamaa hawa noma moja wao kafanana na machalii wa laurel n hardy wanachekesha kinoma
 
 
+1 #2 kabakufa 2011-01-21 13:08
umoja ni nguvu wanangu cha msingi nikuweka tofauti pembeni na kulisimamisha kundi,tuongeze mishemishe za maisha kujiongezea kipato na tusitegemee mziki zaidi,bongo bado magumashi kila pembe,poa pamoja sana
 
 
-1 #1 emma 2011-01-18 12:05
wameptelea wapi hawa watu
 

Weka Maoni

Security code
Upya

BONGO WIKI HII

ZILIZOTUFIKIA

 1. Rama Dee/G Nako/Pipi
  Make Up

 2. Wakazi
  Deuces Remix

 3. Roselin
  Nimekuchagua

 4. Nevy D
  Cute Girl

 5. Watengwa/Waturu
  Hatujaja Kujaribu
Soma Zaidi...

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.