12 Agosti 2010 |
Ray Mazimba, mmoja wa wahusika katika mchezo wa Wahapahapa, ni DJ maarufu katika radio ya Masifa FM iliyoko huko Kalumbi. Katika radio hii Ray anaendesha kipindi maarufu kinachojulikana kama “Mwale wa Jua”. Kila wiki Ray anasaka na kufanya mahojiano na mmoja wa wanamuziki maarufu wa Kitanzania katika kipindi hiki.
   
Kwa kutumia kipindi hiki Ray anawapa wasikilizaji fursa ya kusikiliza wasanii hawa wakiimba nyimbo zao maarufu moja kwa moja toka studio na baadae kusikiliza nyimbo zilizorekodiwa kwenye santuri zao.
Kipindi hiki cha Mwale wa Jua kinayo kimepewa haki kisheria, toka kwa wanamuziki wenyewe, ya kukusanya nyimbo zao zilizotumikak kwenye kipindi hiki na kutengeneza albamu moja mara nne kwa mwaka na hatimae kuzisambaza kwa wapenzi wa muziki kupitia msambazaji maarufu hapa Tanzania, GMC Records. Albamu hizi zinapatikana Tanzania nzima. Unaweza kusikiliza albamu hizi kwa kubofya katika vipicha hapo juu. Utaweza kusikiliza nyimbo za injili, rege, bongo flava, na bendi.
Pia unaweza kusikiliza mahojiano ya kipindi hiki cha Mwale wa Jua hapo chini
|
Maoni
RSS