Februari 23, 2008, STRADCOM waliandaa tamasha kubwa la muziki ili kutangaza mradi wake wa mchezo wa radio ujulikanao kama “Mchezo wa Wahapahapa”. Mashabiki wasiopungua elfu nane walishuhudia wanamuziki maahiri wa Kitanzania ‘wakifunga’ kazi jukwaani.
Wanamuziki waliokuwa wakilisakanyua jukwaa la tamasha hilo walikuwa ni Juma Nature (Bongo flavor), Mlimani Park Orchestra (Congo Dance), Flora Mbasha (Injili), Banana Zorro (Bongo Flavour) na Wahapahapa Band (TanzRock).
Kutoka katika tamasha hili kubwa, kilitengenezwa kipindi maalum kilichorushwa katika luninga pamoja na video ya muziki wa jukwaani.
Unaweza kubofya viunganishi hapo chini kutazama sehemu ya tamasha hilo.
|