Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?

Je kuna msanii unayemfahamu na hayuko kwenye wavuti yetu? BOFYA HAPA KUMUWEKA

Mlimani Park Ochestra

Jaribu kufikiria ukiweza, bendi yenye wanamuziki nguli kama Bob Dylan na Leonard Cohen kama waimbaji watangulizi wakishereheshwa na bendi ya JBs ambayo james brown alirekodi nay o wimbo wake wa 'sex machine'. Kwa watanzania Mlimani Park Orchestra ni kama bendi hiyo. Bendi hii inaongozwa na waimbaji waongozaji wawili, Hassani Bitchuka na Cosmas Tobias, na kusaidiwa na wenzao ktk 'idara' ya vyombo na sauti murua na kuifanya kuwa mojawapo ya bendi maarufu katika ukanda wa afrika mashariki.

Mlimani Park Orchestra ilianzishwa mwaka 1978 katika kitongoji cha Mwenge katika jiji la Dar. Thobias Chidumule ni mmojawapo ya wanamuziki waanzilishi wa bendi hii na alikuwa namna pekee ya utunzi na uandikaji wa nyimbo zake kwa namna ambayo alitaka kuwasilisha ujumbe kwa hadhira yake. Akionesha ukomavu wake kama vile mwalimu anavyoweza kufanya kwa wanafunzi wake tobias aliwagusa wengi kwa tungo zake na muziki safi. Nyimbo kama "Mtoto Akililia Wembe" na Usitumie Pesa Kama Fimbo" zinaonyesha namna ambavyo alikuwa na ueledi na falsafa ya hali ya juu ktk maisha.

Hata hivyo bendi hii haikuwa maarufu mpaka Bichuka alipojiunga nayo miaka ya mwanzo ya 80. Hassan Bichuka alikuwwamtulivu na mwenye ushawishi mkubwa kwenye bendi. Sauti yake ni ya juu, tulivu na yenye kuleta utofauti na ya Tobias ambaye huimba kwa hisia kali za mwili na kuzihamishia kwenda kwenye sauti inayobadilika na kuwa ya juu. Pamoja na kuwa na sauti iliyotulia tungo za Bichuka ni za kimapenzi zaidi na kibinafsi tofauti na Tobias ambaye tungo zake zinajikita kisiasa zaidi. Baadhi ya tungo za Bichuka alipokuwa na Mlimani Park zinazopendwa zaidi ni 'fikirini nisamehe' na 'neema'. Neema uliweza kushika nafasi ya kwanza kama muziki bora wa mwaka kwa miaka miwili mfululizo (1985-1986). Wimbo huu unaonesha ukomavu wa utunzi wa nyimbo za kitanzania.

Mwanamuziki mwenye kipaji zaidi katika bendi ni Michael Enoch, mpiga gita wa zamani wa Dar jazz band ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa bendi hiyo kabla hajahamia Mlimani Park Ochestra. Huyu ndiye hufanya maamuzi ya mwisho juu ya mpangilio wa muziki japo wanamuziki wengine nao wanaruhusiwa kukuonesha ubunifu wao. Si jambo la ajabu kumkuta Enoch akiwa jukwaani akiwaongoza wenzake kukung'uta gitaa la solo ktk nyimbo ambazo ameshiriki kuzipangilia. Kwa kawaida si rahisi kwa wanamuziki nguli kufanya kazi pamoja. Hivyo Tobias na Bichuka wamewahi kuihama bendi hii ktk vipindi tofauti na kurejea katika vipindi tofauti. Kwa sasa Bichuka yupo na Tobias hayuko tena na bendi hii. Hata hivyo pamoja na hayo muziki wa Mlimani Park utaendelea kusikika ktk kumbi mbalimbali za muziki Tanzania. Kuna albamu yenye mkusanyiko wa nyimbo za Mlimani Park toka Radio Tanzania inapatikana na si vibaya kujipatia nakala yako.

 

Maoni  

 
0 #4 Danielbooft 2018-12-22 00:08
buy cialis
buy cialis
buy viagra
buy viagra
buy cialis
buy cialis
buy viagra
buy viagra
 
 
0 #3 Timothyartex 2018-12-21 17:12
buy cialis
buy cialis
buy viagra
buy viagra
buy cialis
buy cialis
buy viagra
buy viagra
 
 
0 #2 Ilse 2016-08-05 12:09
Tɦiѕ mɑy Ƅecome performing սp for a survey ɑnd posting youг email
address, house address аnd afteг thɑt completing offerѕ that require yoᥙ to mаke purchases
օr asкing you fⲟr your mobile strike free gold
hack tool
Strike accounts, iTunes account оr Google Play
account.
 
 
0 #1 Mireya 2016-04-12 22:03
Disclaimer: mobile strike hack free unlimited gold gold and
vip
Strike Crack Device and Secrets
and cheats is usually for educational purpose only.
 

Weka Maoni

Security code
Upya

BONGO WIKI HII

ZILIZOTUFIKIA

 1. Rama Dee/G Nako/Pipi
  Make Up

 2. Wakazi
  Deuces Remix

 3. Roselin
  Nimekuchagua

 4. Nevy D
  Cute Girl

 5. Watengwa/Waturu
  Hatujaja Kujaribu
Soma Zaidi...

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.