Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?

Je kuna msanii unayemfahamu na hayuko kwenye wavuti yetu? BOFYA HAPA KUMUWEKA

Bi Kidude

Bi. Kidude binti Baraka na mwanamuziki mkongwe sana katika tasnia ya Muziki wa Mwambao (Taarab). Bibi huyu ana maskani yake huko visiwa vya Zanzibar. Akizungumzia historia yake ya muziki anasema alianza kuimba tangu akiwa na miaka kumi, na katika umri huo alikuwa tayari ameshaanza kusafiri kwenda kurekodi nyimbo zake huko nchini India, akitumia usafri wa majahazi ya waarabu.

Hakuna anayejua umri kamili wa Bi. Kidude na hata historia yake ya muziki imejificha sana, kwani hakuna ambaye amewahi kuiandika mahala, hali hii inazidi kumfanya Bi. Kidude kuwa mwanamuziki ambaye watu wanaichimba zaidi safari yake ya muziki ili kufahamu hili na lile. Ila kuna jambo moja ambalo li wazi, Bi Kidude ni mwanafunzi wa muziki wa Taarab toka kwa mkali mwingine wa muziki huo, Siti bint Saad.


Bi Kidude amerindima muziki wake Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, na hata Japan. alifanikiwa kurekodi albamu yake ya kwanza katika kipindi cha kama miaka 10 hivi iliyopita na akaipa jina la "Zanzibar", hapo alikuwa na umri unaosadikika kuwa miaka isiyopungua 80. Pia ameshafanya kazi na mastudio makubwa duniani kama  Retro-Afric, Piranha, Globestyle, Jahazi, even EMI/Virgin.

Hatimae, siku za hivi karibuni akafanikiwa kurekodi albamu yake ya nyingine akiwa nyumbani, "Machozi ya Huba", katika studio za Heartbeat Records.

 

 


Pamoja na kuwa msanii mkubwa wa muziki wa Taarab katika Afrika na hata dunia, Bi. Kidude bado haachi asili kwani pia huwa anaburudisha katika shughuli za unyago huko nyumbani kwao Zanzibar. Akiwa anakaribia miaka 100 sasa, bibi huyu bado ni kitambulisho maridhawa cha utamaduni wa Zanzibar, akifunda wanawake juu ya ngono salama na madhara ya ngono lazimishi na zembe.

Mwaka 2005 Bi Kidude alitunukiwa tuzo ya mafanikio ya maisha ya World Music Expo (WOMEX). Mwanamuziki mkubwa kabisa duniani alisema maneno yafuatayo wakati wa kukabidhi tuzo, "the singer, well in her nineties yet still sporting a bone-crushing handshake, received the honours in recognition of her more than 80 years of singing and serving as a cultural mediator and advisor of the younger generations, including on matters of sex and marriage - a proper symbol of World Music's emancipatory, liberating and strengthening power."

 

 

Maoni  

 
0 #8 Leoma 2017-04-11 02:12
Driver update software takes the guess work and frustration away from downloading and installing updates
and is also quite easy and easy to make use of and finds, downloads and installs any update you need.
That is, should you be just like a large amount of people that depend on their PC's and printers for professional or business means,
from date drivers can simply lead to one's printing setup or data transference actions to fail apparently from the nowhere.
This is dubstep vol 3 rar -
this is dubstep vol 3 rar
warning will advise you if
ink or toner is low, and this will specify whether you need to replace the
black or color cartridge.
 
 
0 #7 Son 2017-04-10 15:49
For example, many video cards and printers have basic software for governing the
device. As any driver gets more out dated, the end consequence
that can result, is only the certain little bit of hardware ceases to function whatsoever.
The first step is to locate the manufacturer's web site, that ought
to be as elementary as adding a dot com towards the manufacturer
within an address bar or searching inside your favorite search engine.


Here is my blog - Alliedmodders sound commands
 
 
0 #6 Kristopher 2016-01-10 01:36
Ahaa, its nice conversation on the topic of this paragraph here at this blog,
I have read all that, so now me also commenting at this place.


Look into my web site ... royalty free news footage
 
 
+5 #5 mabovu 2011-02-28 14:09
Bi kidude apumzike sasa aachie damu changa
 
 
0 #4 man chidi 2011-01-23 10:52
Tunawaomba waheshimiwa muweke page ajili ya wasanii wanaochipukia
 
 
0 #3 kishe 2010-11-22 08:44
bikidude umefunika san a hasa enzi zako sasa pumzika waachie vijana wewe ubakikua mshauritu
 
 
+1 #2 bonge haule 2010-11-15 14:07
ila tishio kwa watoto wanakuwa wapole wakimuona!
 
 
+1 #1 rebeca 2010-11-10 17:05
Mungu amzindishie maisha marefu
 

Weka Maoni

Security code
Upya

BONGO WIKI HII

ZILIZOTUFIKIA

 1. Rama Dee/G Nako/Pipi
  Make Up

 2. Wakazi
  Deuces Remix

 3. Roselin
  Nimekuchagua

 4. Nevy D
  Cute Girl

 5. Watengwa/Waturu
  Hatujaja Kujaribu
Soma Zaidi...

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.