Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?

Je kuna msanii unayemfahamu na hayuko kwenye wavuti yetu? BOFYA HAPA KUMUWEKA

Soggy Doggy

Wiki hii ni zamu ya msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Anselm Ngaiza ‘Soggy Doggy au Chief Rumanyika ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Uhuru cha jijini Dar es Salaam. Hapa anajibu na kufafanua juu ya yale mliyomuuliza.

Mbona kimya?
Mbona upo kimya katika muziki au ndiyo umeutupia kushoto? Msomaji, 0654857882.

SOGGY: Sijautupa muziki ila nilikuwa nimepumzika, nitarudi na utanisikia hivi karibuni.

Ni Mhaya na Mluguru
Soggy ni mchanganyiko wa Kabila la Mhaya na Mluguru, kimuziki mbona ameshuka sana? Cassian, 0655202202.

SOGGY: Mimi Mhaya na sitegemei muziki pekee kwa hiyo lazima nishuke.

Ufagio
Kiukweli nakukubali sana wewe pamoja na kipindi chako cha Uhuru Fleva, Dorice, Dar, 0714251076.

SOGGY: Nashukuru sana.

Huyu kajichanganya
Namfahamu Soggy toka anasoma Sangu Mbeya, ni nani aliyekupa jina la Soggy? Last Voice, Mbeya, 0755022486.

SOGGY:
Sijasoma Sangu, mimi nilisoma Meta Mbeya na jina la Soggy nilipewa na wanafunzi wenzangu.

Msaada kimuziki
Napenda jinsi unavyoimba, siyo siri na mimi ningependa unifundishe kuimba. Riham, Dar, 0767444404.

SOGGY: Asante, usijali tuwasiliane.

Msanii anayemkubali
Soggy ni msanii gani unayemkubali wa hapa nyumbani na kwa nje ya Bongo? Pius, Moshi, 0717679047.

SOGGY: Wapo wengi.

Huyu anamjua
Mimi namjua Soggy alishawahi kuwa na uhusiano na dada mmoja anaitwa Devota ni Mhaya. Devota ni rafiki wa Aisha Masa. Kibajaji, Dar, 0786371246.

SOGGY: Ni kweli.

Mbona kimya, umeoa nini?
Kaka mbona haupo hewani? Mimi ni mpenzi wa muziki wako au umeoa? Tunu, Tanga, 0712007388.

SOGGY: Ndiyo nimeoa na hewani nipo bahati mbaya hunisikii.

Kuhusu Hot pot
Mimi namfahamu kitambo Soggy, vipi kuhusu Hot Pot Family na mshikaji wake Suma G, mbona kimya? Chalz, Dar, 0714683500.

SOGGY: Tunajipanga utatusikia hivi karibuni.

Kazi anayoipenda zaidi
Ni fani gani unayoipenda zaidi kati ya zote mbili unazozifanya? Nizar Mafita, Dar, 0653485444

SOGGY: Napenda zaidi kuimba kuliko kutangaza.

Ufagio
Kaka nakufagilia hasa Kipindi cha Old School za Kibongo kila Jumatano ila vile vioja kama vya RFA (Redio Free Africa) sisikii siku hizi! Msomaji, 0714892412

SOGGY: RFA nilikuwa mtoto, sasa hivi nimekua.

 


Mshika mawili
Wanasema mshika mawili moja humponyoka, unawezaje kumudu utangazaji na muziki? China, Moshi, 0754664097.

SOGGY: Utangazaji nimesomea na muziki ni kipaji nilichozaliwa nacho kwa hiyo hainipi shida.

Eti kaachana na muziki!
Nasikia umeamua kuachana na muziki baada ya kuona wasanii wa sasa wanabana kila upande. Noel Willz, Mbeya, 0757129125.

SOGGY: Sijaacha muziki na siwezi kuacha, tumelianzisha na tutalimalizia wenyewe.

Huyu anamjua vizuri
Ulisoma Jitegemee Sekondari enzi zile za Mwalimu Mkuu Masawe, ulikuwa unampenda sana msichana mmoja anaitwa Kulwa, tena ulikuwa naye karibu sana. Msomaji, 0715584148.

SOGGY: Kweli Kulwa namjua na nilikuwa naye darasa moja. Sijawahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Wimbo anaoupenda zaidi
Wimbo gani unaupenda kuliko nyimbo zako zote? Jofrey, Turiani, 0712853696.

SOGGY: Wimbo wa Stori ndiyo naupenda zaidi.

Aliyempa jina la Soggy
Jina la Soggy Dogg alibatizwa na mwalimu wake huko Mbeya alipokuwa anasoma sekondari.
J. Ipemba, Shinyanga, 0713554815.
SOGGY ANAJIBU: Jina la Soggy nilipewa na wanafunzi wenzangu, siyo mwalimu.

Yuko juu
Nakukubali kaka Soggy uko juu una sauti bomba, Arusha ulifunika redio Tripple A. Mama Gaby, 0715711196.
SOGGY ANAJIBU: Nashukuru sana.

Ni mdogo wa Alex Ngaiza
Namfahamu Soggy, alizaliwa na kuishi Ubungo NHC, kaka yake ni Alex Ngaiza. Khadija Bunto, Dar, 0716317251.
SOGGY ANAJIBU: Ni kweli.

Mbona kapotea?
Namjua Soggy enzi hizo akiwa na Hot Pot Family, alivuma sana kati ya mwaka 1998 hadi 2004, siku hizi amepotea sana kwenye gemu. Laurian Mboya, Moshi, 0713050545.
SOGGY ANAJIBU: Ni kweli ila nina kazi nyingine mtanisikia tu.

Demu wa kibanda cha simu
Yule msichana aliyemshirikisha kwenye Wimbo wa Kibanda cha Simu ndiye mkewe? Msomaji, 0755779465.
SOGGY ANAJIBU: Yule siyo mke wangu, ni Josephine na ameshaolewa.

Bifu na afande
Aliwahi kuwa na bifu na Afande Sele kwa yeye kuwa Mfalme wa Rhymes. Gift Masawe, Moshi, 0756418672.
SOGGY ANAJIBU: Ni kweli lakini ulikuwa ni utoto tu.

Anakubalika
Soggy nakukubali mtu wangu, achia kibao kikali kushinda kile cha Kibanda cha Simu. Dismas John, Tanga, 0712080954.
SOGGY ANAJIBU: Usijali, muda utafika.

Historia yake
Vipi mkubwa, naomba historia yako. Claud, Moshi, 0769169396.
SOGGY ANAJIBU: Historia yangu ni ndefu sana, nitajaza ukurasa.

VIPI KUHUSU KUFUFUA HOT POT FAMILY?
Kaka vipi kuhusu muziki? Je, utafufua kundi lako la Hot Pot Family? Clement, Arusha, 0652641056.
SOGGY ANAJIBU: Kundi halijafa bado lipo mtatusikia hivi karibuni.

Habari kwa hisani ya gp

 

Maoni  

 
0 #1 said 2011-04-24 20:12
duh! kaka vp mbona kimya kinazidi sana tumemisi vituvyako kaka hebu udhihirishie uma kama bado upo kwenye gemu
 

Weka Maoni

Security code
Upya

BONGO WIKI HII

ZILIZOTUFIKIA

 1. Rama Dee/G Nako/Pipi
  Make Up

 2. Wakazi
  Deuces Remix

 3. Roselin
  Nimekuchagua

 4. Nevy D
  Cute Girl

 5. Watengwa/Waturu
  Hatujaja Kujaribu
Soma Zaidi...

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.