Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?

Je kuna msanii unayemfahamu na hayuko kwenye wavuti yetu? BOFYA HAPA KUMUWEKA

Galinoma

Wiki hii tunaye msanii wa muziki wa Reggae aliyejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi anayekwenda kwa jina la Innocent Galinoma (pichani).

Alizaliwa Aprili 30, mwaka 1960 mkoani, Iringa Kijiji cha Karangu. Elimu ya msingi aliipata katika shule tofauti zikiwemo Muhimbili na Kinondoni.

Alipomaliza darasa la saba alijiunga na Sekondari ya Shaban Robert ya jijini Dar es Salaam.Baada ya kuhitimu kidato cha nne alifanikiwa kulamba ajira katika Benki ya NBC kabla ya kwenda nchini Marekani

TQ: Kwa maana hiyo muziki ulianza lini hasa na nini kilichokusukuma kuingia huko?
Galinoma: Ilikuwa mwaka 1975. Kilichonishawishi kuingia kwenye muziki ni mambo ya ubaguzi wa rangi yaliyokuwa yakichukua nafasi katika baadhi ya nchi za Afrika.

TQ: Kumbe muda mrefu sana umeanza kufanya muziki! Ni mafanikio gani umeyapata kupitia fani hiyo?
Galinoma: Kwanza maisha yangu ni mazuri, wanangu wote nawasomesha nchini Marekani. Hata hivyo, sipigi muziki kimasilahi bali kikubwa nataka kuisaidia jamii yangu.

TQ: Ni malengo gani uliyonayo katika siku zinazokuja?
Galinoma: Nimejipanga kuanzisha kitu ambacho kinahusiana na muziki wa reggae, wakati ukifika nitawataarifu.

TQ: Kuna vijana wanalalamika muziki wa Hip Hop Bongo haulipi, vipi reggae inalipa?
Galinoma:  Inalipa lakini siyo kama miziki mingine ya msanii kutembea na CD mfukoni.

TQ: Mbali na muziki, kuna shughuli nyingine unafanya?
Galinoma: Mimi ni mchoraji ingawa siwezi kujisifia sana lakini angalau najitahidi.

TQ: Vipi kuhusu maisha ya kimapenzi, umeoa?
Galinoma: Nimeoa kwa mkataba. Nimejaaliwa kupata watoto wanne ambao  wanasoma Marekani.

TQ: Unawashauri nini wasanii wenzako ili kuweza kupata mafanikio makubwa kupitia muziki?
Galinoma: Siwezi kuwashauri chochote kwani mi mwenyewe nahitaji ushauri ila nawaomba waaache kupiga muziki wa kutengenezwa kwenye kompyuta.

TQ: Ni msanii gani ambaye unamkubali sana?
Galinoma: Licha ya kwamba ni marehemu lakini namkubali sana Bob Marley. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.

TQ: Mbali na reggae ni muziki gani mwingine ambao ukipigwa unajisikia raha.
Galinoma: Bendi kama vile Sikinde, Msondo, Kilwa Jazz ‘nazi-feel’ sana. Hawa wanaimba nyimbo tangu enzi zile lakini bado zinakubalika hadi leo. Kwa mfano wimbo wa Asma wa Sikinde, ukiusikiliza lazima ulie, hiyo ndiyo miziki ninayopenda kusikiliza.

TQ:Unalizungumziaje Tamasha la Uzalendo litakalofanyika kesho pale Biafra Kinondoni?
Galinoma:Siwezi kuzungumza sana kuhusiana na hilo ila ninachowaomba watu wafike kwa wingi washuhudie elimu pamoja na burudani, siyo siku ya kukosa.

 

Weka Maoni

Security code
Upya

BONGO WIKI HII

ZILIZOTUFIKIA

 1. Rama Dee/G Nako/Pipi
  Make Up

 2. Wakazi
  Deuces Remix

 3. Roselin
  Nimekuchagua

 4. Nevy D
  Cute Girl

 5. Watengwa/Waturu
  Hatujaja Kujaribu
Soma Zaidi...

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.