Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
27 Juni 2011

Shaggy Asimikwa Uchifu Mwanza

Shaggy Asimikwa Uchifu Mwanza

MWANAMUZIKI wa Marekani, Shaggy, jana aliachwa hoi na Wasukuma baada ya kumkabidhi vifaa vya asili vya utamaduni wa kabila hilo.

Shaggy alikabidhiwa mkuki, fimbo, usinga, kaniki na machifu wa kabila la Kisukuma, wakiongozwa na Mark Bomani.

Shaggy alikabidhiwa vifaa hivyo katika sherehe ya ngoma za asili ya Kisukuma, inayofanyika Bujora nje kidogo ya jiji la Mwanza.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Bomani alisema kuwa vifaa hivyo mkuki na fimbo ni silaha za jadi kwa ajili ya kujilinda yeye pamoja na jamii ya Kisukuma.

“Hivi tunavyokukabidhi leo ni ishara ya kukukaribisha katika ardhi ya Wasukuma na ni kukuonyesha Wasukumaa wana kukubali na wanakupenda,” alisema Bomani ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Bia ya Serengeti.

Bomani alisema kuwa Wasukuma wameamua kumpatia vifaa hivyo, ikiwa ni ishara ya kumkaribisha.

Akizungumza na wananchi wakazi wa Mwanza, waliojitokeza kwenye sherehe hizo, Shaggy alisema kuwa ameshangazwa na mambo anayofanyiwa na wananchi wa Tanzania tangu alipotua nchini.

Alisema kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania pindi atakapoondoka, ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio ambavyo Tanzania imebarikiwa kuwa navyo.

na Khadija Kalili, Mwanza

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.