Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
22 Machi 2011

Sikinde Kumtoa Jumbe Kimasomaso 22 MACHI 2011

Sikinde Ngoma ya Ukae

BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Mlimani Park 'Sikinde Ngoma ya Ukae' imepanga kutumia maonyesho yake ya wiki hii kumtambulisha mwanamuziki wake iliyemrejesha kundini Hussein Jumbe.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salama jana Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Sikinde, Jimmy Chika, alisema kuwa wamepanga kumtambulisha Jumbe katika bonanza litakalofanyika Jumamosi hii kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo na Jumapili mchana katika bonanza lao kwenye ukumbi wa TCC Club-Chang’ombe.

Alisema kuwa Jumbe aliyerejea siku moja kabla ya kuwavaa mahasimu wao Msondo katika mpambano uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee wikiendi iliyopita, ameanza mazoezi na wenzake kuandaa albamu mpya.

“Tunapenda kuwaambia wapenzi wa Sikinde wafike katika maonyeshio yetu ya wiki hii ambapo tutamtambulisha Hussein Jumbe ambaye amerejea kundini baada ya kuwa nje kwa muda,” alisema Chika.

Alisema mbali ya kumtambulisha katika maonyesho hayo ya bonanza lakini pia watamtambulisha rasmi kwa mashabiki watakaohudhuria onyesho lao kwenye ukumbi wao wa nyumbani wa SUWATA, ulioko Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Jumapili usiku.

 

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.