Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
24 Machi 2011

Sharobaro President vs Rais wa Watanashati Kili Awards

Sharobaro President vs Rais wa Watanashati Kili Awards

Ni mara nyingi hapa nyumbani wasanii wetu hugeukana mapema zaidi ama kwenye makundi au  kwenye mikataiba tofauti na wenzao wa nje, ila mwaka huu KILI AWARDS imetutegeshea kabisa kamchezo ambako walikaanzisha wenyewe wasanii hao sasa sisi wapenzi wao wa mziki tupanganue wenyewe.

BOB JUNIOR na DIAMOND ama Naseeb wanawania nafasi moja ya kipengele cha WIMBO BORA WA AFRO POP,  wawili hawa waliwahi kufanya kazi nzuri kwa pamoja, huku Diamond akiwa mwimbaji na Bob Junior akiwa prodyuza, sasa leo hii wanawania nafasi moja, kwani Bob Junior kaingia kwenye kuimba pia, na nyimbo anayoshindania ni OYOYO, huku Diamond akiwania na nyimbo ya Mbagala.

Wasani hawa wamefikia hadi kutupiana maneno kwenye vyombo vya habari, huku mmoja akijiita SHAROBARO  PRESIDENT, na mwenzie akijiita PRESIDENT WA WATANASHATI.

Amini usiamini mpenzi msomaji lakini kinyanganyiro chao hakiishi kwa wawili hao tu, bali ni kikali sana, kwani wasanii ambao pia wanagombea nafasi hiyo ni pamoja na wale walioimba nyimbo ya MAMA NTILIE wa Gelly wa Rhymes akiwashirikisha akina  RAY C na  AT.

Lakini mbali na kundi hilo, kuna msanii anaezidi kujipatia heshima kwa kutoa nyimbo zenye kutuma ujumbe wenye uhalisia wa maisha, nae ni 20%. Kijana huyo ameingia kwenye kinyanyanyiro na nyimbo zake 2 ambazo hata wewe lazima uliwahi kukaa na kuzisikiliza kwa makini kwani maneno yaliyo ndani ya vina hivyo ni vyenye busara, nazo nyimbo hizo ni YA NINI MALUMBANO na TAMAA MBAYA.

Tukae mkao wa kula tujue nani zaidi ya nani.

Habari na Kulthum Maabad

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.