Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
24 Machi 2011

Khadija Kopa Chupuchupu Ajali ya 5 Star

Kopa 5 Star

Baada ya kupata Taarifa za msiba mzito wa wasani wetu mashuhuri wa 5 STAR uliotokana na ajali mbaya iliyotokea Usiku wa Saa 2 Tarehe 21/02/2011 katika barabara kuu ya Iringa-Morogoro kwenye eneo la Hifadhi ya Wanyama ya Mikumi na kusababisha vifo vya watu 13 na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya.

Habari zilizotujia baadae ni pamoja na ile ya kuponea chupuchupu kwa ajali hiyo mbaya kabisa kwa msani Gwiji wa muziki wa Taarab bi Hadija Kopa, akielezea mwenyewe huku akiwa na masikitiko makubwa ya msiba wa wenzake hao, Bi Hadija alisema kuwa siku chache kabla ya ajali hiyo alipigiwa simu na kiongozi wa bendi hiyo kuwa aungane nao kwa ajili ya onyesho huko mkoani ila alimweleza kuwa asingeweza kwani alikuwa amebanwa na mambo mengine hapa jijini Dar es salaam, sababu ambayo leo hi ndiyo iliyomnusuru kifo ama majeraha makubwa kama angejumuika nao.

Bi Hadija Kopa ni miongoni mwa Waanzilishi wa mitindo taarabu ya mipasho na kupelekea kubadilika kwa taarabu asilia na mwishowe kupewa jina la Modern Taarab akiwa pamoja na mkali mwenzake marehemu Nasma Hamisi.

Ajali hiyo mbaya ilitokana na mwendo mkali wa gari la wasani hao kupelekea kugonga semitrela lilokuwa limebeba mbao na kubandua ubavu wa kushoto wa gari hilo kuacha upande wa dereva ambae alibahatika kupona.

Msiba huu ni wa watanzania wote kwani pengo hilo waliloliacha halizibiki kamwe, Raisi wetu JK ametoa rambirambi zake kupitia kwa Waziri wake wa vijana, habari, michezo na utamaduni

“Binafsi nimeguswa mno na msiba huu kwa vile umetupotezea wasanii ambao walikuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza sanaa ya muziki wa Taarab nchini kwetu. Hili ni pigo kubwa siyo kwa usanii wa Taarab bali kwa Taifa letu zima la Tanzania.” Amesema Rais Kikwete katika salamu zake.

Nalo baraza la sanaa Tanzania limetoa rambirambi zao ikiwa ni pamoja na shilingi laki 5 za kusaidiwa mazishi. 5 STAR hapo mwaka jana kwenye KILI AWARDS iliweza kuingia kwenye kinyanganyiro cha kuwania nafasi ya albamu kali ya Taarab ikiitwa Riziki mwanzo wa Chuki.

Tanzania imekuwa mpenzi wa muziki aina ya Taarab hasa sehemu za pwani tokea enzi na enzi,ilikuwa hivyo hata kabla ya kuingia kwa muziki wa dansi ambao ulianzia kule congo baada ya vita vya pili vya dunia mwaka 1945.

Taarab hiyo ilifanikiwa kuingia hapa nchini kwa uraisi kutokana na ukaribu kati ya waarabu na wenyeji na pia upatikanaji wa vyombo vyake vya muziki kwani vingi vilikuwa vikitengenezwa na mwimbaji mwenyewe kutoka kwenye vitu asilia tofauti na muziki wa dansi ambao vyombo vyake ni vya kisasa zaidi na vingi vyenye kutumia umeme.

Kwa bahati mbaya au nzuri taarabu hiyo ya zamani imefunikwa na aina mpya ya Taarab hapa nchini yenye wapenzi ambao ni vijana zaidi na kufikia kuipa jina la MODERN TAARAB, mabadiliko hayo ni pamoja nayale ya uandishi wa nyimbo mpaka vyombo vya kupigia muziki huo.

Hata uchezaji nao ni tofauti, kwani ilizoeleka wana cheza wakina dada pekee tena kwenye miduara lakini sasa hata wanaume wanamiminika kwenye dance floor, na pia midundo inaenda ikikaribia kufanana kwa mbali na ile ya dansi, hali inayofanya uweze kuucheza mziki huo wa modern taarab kama unavyocheza tu nyimbo zozote za hapa nyumbani.

Baada ya kukuhabarisha kwa yote hapo juu basi nasisis wana wahapahapa hatuna budi ila kutoa salamu zetu za rambi rambi kwa ndugu jama, marafiki pamoja na wapenzi wa muziki wa 5 STAR, mungu azilaze miili yao paali pema peponi, Ameen.

Kulthum Maabad

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.