Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
24 Machi 2011

Wazee wa Ngwasuma Kufyatua Mpya

FM Academia

BENDI ya mahiri ya muziki wa dansi nchini, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ imeanza maandalizi ya albamu yao ya mwaka 2012.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El Sadat alisema, tayari wameishaanza mazoezi ya maandalizi ya albamu hiyo ambayo yanafanyika mara mbili kwa wiki katika ukumbi wa New Msasani Club.

Nyoshi alisema albamu hiyo itajulikana kwa jina la ‘Chuki ya Nini’, ambapo alisema jina hilo linatokana na wimbo wa chuki ya nini ambao umetungwa na yeye mwenyewe Nyoshi.

“Kama ulivyosikia ni kweli bendi yetu imeanza maandalizi ya albamu hiyo ambayo itabeba jumla ya nyimbo 12, ambapo karibu kila mwanamuziki ametunga wimbo wake hivyo tunawaambia mashabiki wetu wakae mkao wa kula, kwani tupo jikoni tayari kwa ajili ya kuipika albamu hiyo ambayo itakuwa ni kabambe ...ila wakati tunaendelea na maandalizi hayo tunaomba waendelee kuifurahia albamu ya vuta ni kuvute,” alisema Nyoshi El Sadati.

na Happiness Katabazi

1 maoni

  • Maoni george mopao mtoto ya mungu 25 Machi 2011 george mopao mtoto ya mungu

    isiwe ya haraka sana tunaitaji ladha tofauti tofauti kwa sauti ngeni kama ilivyo kuwa dunia kigeugeu

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.