17 Juni 2011

Jose Awapotezea Wazee wa Ngwasuma

Jose Awapotezea Wazee wa Ngwasuma

Mwanamuziki mwenye sauti mwanana na yenye mvuto wa kipekee wa bendi ya FM Academia aka Wazee wa Ngwasuma, Jose Mara amejiondoa rasmi katika bendi hiyo.

Taarifa zilizofika mezani kwetu zimeweka wazi kuwa Jose Mara au maarufu kwa jina la 'Josee' amejitoa FM Academia ili kuweza kuitumikia vyema bendi yake ya Mapacha Watatu akiwa na wachapakazi wenzake kina Khalid Chokoraa na Kalala Junior.

Bendi ya Mapacha Watatu iliyoanza kama bendi ya 'zing zong' imejipatia umaarufu kwa muda mfupi kutokana na kupiga muziki wenye midundo mchanganyiko na hivyo kujizolea mashabiki kibao.