27 Juni 2011

Ajali Yamkuba Kiba

Ajali Yamkuba Kiba

Blogu ya Bongo Star Link inaandika: Habari zilizonifikia zinasema kuwa msanii wa bongo fleva Ally Kiba amepata ajali maeneo ya Mikumi Morogoro akiwa anatokea MBEYA akiwa na steji show wake.

Nimeongea na Ally Kiba akaniambia alikuwa na show Mbeya na baada ya kumaliza show hiyo ilibidi waondoke na kurudi Dar ili aweze kupanda ndege na kuelekea Mwanza kwenye FIESTA.

Kwenye majira ya saa 11 asubuhi wakati wanakatiza Mikumi ndipo gari hilo dogo ilipopata ajali, Kiba anasema hakujua jinsi ajali hiyo ilivyotokea kwa sababu kulikuwa na giza, ila inasemekana dereva alikuwa amelala maana hakupumziki na Kiba alimwambia kama amechoka ampe yeye gari aendeshe lakini jamaa alikuwa mbishi na matokeo yake kuwa hivyo. Kiba ameumia kwenye mguu na mkono na kwa sasa yupo nyumbani kwao Dar na anaenelea vizuri.