Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
27 Juni 2011

Elephant Man Funiko Bovu Str8Muzik Beach Party

Elephant Man Funiko Bovu Str8Muzik Beach Party

MAMIA ya mashabiki wa burudani, walijimwaga na kuselebuka kwenye Club ya Mbalamwezi Beach jijini Dar es Salaam kushiriki Tamasha la Str8Muzik Beach Party 2011, ambako kulikuwa na mgeni wa kipekee, ambaye ni mwanamuziki wa kimataifa, Elephant Man aliyekonga nyoyo za mashabiki.

Nyota huyo, mwimbaji wa muziki wa Dancehall Reggae, Elephant Man ambaye kimataifa pia hujulikana kama Energy God (Mungu wa Nguvu), alipanda kilingeni dakika chache baada ya kutimia saa 4:00 usiku na kutoa shoo ya nguvu kwa saa kadhaa, akiwaacha mashabiki wakicheza muziki na kutabasamu na hata wengine kupiga miluzi kutokana na jinsi alivyowakosha.

Msanii huyo, alikuwa katika mwonekano wa pekee, akionekana kuwafurahia mashabiki waliojitokeza na kisha akaanza kumwaga sifa, akieleza jinsi Dar es Salaam ilivyo nzuri, lakini akisisitiza kwamba, yeye anapiga muziki kwa ajili ya dunia nzima.

“Afrika ni nzuri, Tanzania ni kubwa, kuna vimwana wa ajabu wa Kiafrika,” alikuwa ‘akifoka’ hivyo mara kwa mara.

Msanii huyo aliyejaliwa msuli wa haja, aliimba na kucheza katika miondoko tofauti, ikiwa ni pamoja na sweet reggae, dance reggae na mchanganyiko wa slow sweet reggae.

Alitambua umaarufu wa Buju Banton, anayetumikia kifungo jela nchini Jamaica. Pia aliimba wimbo wa Michael Jackson uitwao ‘We are the World’, katika aina ya pekee ya ‘sweet reggae’, akihitimisha makamuzi yaliyodumu kwa saa moja na nusu.

Utamu zaidi ulinogeshwa na jinsi jukwaa lilivyopangwa kiaina yake kando ya bahari, huku DJ na kundi lake wakiwa kama meta 40 hivi ambapo washiriki walianza kwa michezo mbalimbali, kama kuendesha boti, soka ya ufukweni, kucheza pool, kuendesha majahazi, wavu na kufyatua maji kama risasi kutoka kwenye bastola na kufanya mandhari yote ya ufukweni hapo kung’ara kadiri mwanga wa mchana ulivyokuwa ukiyoyoma.

Matukio yote hayo ya ufukweni, yaliyoanza asubuhi hadi jioni, yalipangwa vema na kushirikisha wasanii wa Tanzania na Kenya, waliokuwa wakifanya maonesho ya utangulizi, kabla ya msanii huyo maarufu, Elephant Man kupanda jukwaani na kuonesha maajabu ya uwezo wake kimuziki.

Wanamuziki waliotangulia kwenye onesho hilo, ambapo pia walileta ladha halisi ya muziki wa Afrika Mashariki katika usiku huo, walikuwa ni pamoja na washindi wa tamasha la Stre8Muzik Freestyle 2011, wakiwapasha moto mashabiki na kuwakumbusha miziki ya miaka ya 1980 na 1990 pamoja na vibao vipya vya siku hizi ya Reggae na Bongo Flava. Baadhi ya wanamuziki hao ni Cpwa, Fid Q, P-Unit na Red San kutoka Kenya.

rRyxG0V90

Wageni walipoingia na kuelekezwa ufukweni, walikutana na makundi ya vimwana warembo, waliowafanya wakajihisi, bila shaka yoyote, kuwa nyumbani, huku aina mbalimbali za michezo ya Str8Muzik ikiendelea kwa siku nzima hiyo.

“Nimefurahia hii. Ukichanganya uendeshaji boti ambao leo ilikuwa bure, kwa hakika nilijisikia kwamba huu ni mtindo wa Bongo, kwa kweli ulikuwa wakati usio wa kawaida,” alisema mmoja wa washiriki, Alex Mcharo.

Maoni kama hayo, yalitolewa na wengine, kama vile Anastasia Bhoke, ambaye kitaaluma ni mfanyakazi wa benki jijini Dar es Salaam, aliyeshiriki pia katika kuendesha boti.

Str8Muzik Beach Party 2011 iliandaliwa na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia chapa yake ya Sweet Menthol.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.