Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
30 Juni 2011

Ngoma za Asili Zingalipo - BASATA

Ngoma za Asili Zingalipo - BASATA

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limesema ngoma za asili bado zina hadhi na nafasi kubwa katika jamii ingawa kwa maeneo ya mijini mwamko wa sanaa hiyo unaonekana kupungua tofauti na zamani.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya Baraza hilo, Ilala, Sharif Shamba, Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, alisema kwamba ngoma za asili zipo kama kawaida na zimekuwa na nafasi kubwa mikoani, ambako zinavuta watu wengi.

“Kuna matamasha makubwa ya ngoma za asili kama yale ya Makuya, ya kale yanapokutana na ya sasa, Bujora na Chamwino. Matamasha haya yamekuwa yakivuta watu wengi sana, hivyo dhana kwamba ngoma za asili zimetoweka si sahihi,” alisema Materego.

Aliongeza kwamba kinachotokea kwa sasa ni athari za utandawazi kwenye ngoma za asili, ambazo zimebadili upepo wa sanaa hiyo maeneo ya mijini, lakini akasisitiza kwamba bado hata maeneo hayo kuna vikundi vingi vya ngoma za asili vinavyofanya vizuri.

“Utandawazi kwa kiasi fulani, umeathiri ngoma za asili, hasa maeneo ya mijini, lakini bado hata hivyo kuna vikundi vingi Baraza limevisajili na kuvisimamia mijini kama hiki kilichotuburudisha leo cha Jivunie Tanzania,” alisisitiza Materego.

Alitoa wito kwa wakuzaji sanaa, kujikita kwenye kuandaa matamasha mbalimbali ya sanaa za asili ili kuzidi kuisambaza sanaa hiyo ambayo ni muhimu kwa utambulisho wa utamaduni wa Tanzania kwa muda mrefu, ambayo imelijengea heshima taifa.

“Ni kweli tuna matamasha mengi ya ngoma za asili, lakini ni wazi juhudi nyingi zinahitajika ili kujenga mwamko zaidi katika sanaa hizi. Ni muhumu ikaeleweka kwamba, sanaa hizi zinabeba kila kitu ndani ya jamii,” alisisitiza Materego.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kundi la sanaa la Jivunie Tanzania, Mariam Ismail, alisema kwamba Watanzania wasiache kupenda ngoma za asili na kupapatikia vitu vya nje, kwani kufanya hivyo ni kupuuza malezi na historia za jamii zao.

Jukwaa la Sanaa, kila mwisho wa mwezi linapambwa na burudani mbalimbali na kwa Juni, kundi la sanaa la Jivunie Tanzania kutoka Temeke, Dar es Salaam lilitoa burudani kedekede za asili.

1 maoni

  • Maoni Bobito 30 Juni 2011 Bobito

    Hakuna aliyekataa kwamba zipo, tatizo zimekosa dira, zimegandia palepale walipoachia babu zetu, sidhani kama wakiamka leo na kukuta hatua tuliyopiga katika ngoma hizo itawafurahisha.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.