Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
01 Julai 2011

Inakuwaje Wasanii wa Kibonge Hamjiendelezi?

Inakuwaje Wasanii wa Kibonge Hamjiendelezi?

KARIBUNI wapenzi wa safu hii ya Vunja vunja ambayo hukupatia fursa ya kutambua maendeleo ya filamu za hapa nyumbani ikiwa ni pamoja na kuchambua mambo ambayo hayapendezi watazamaji nia ikiwa ni kuwezesha tasnia hii isonge mbele.

Leo katika vunja vunja tutakuwa tukiwavunja waandaaji na waigizaji ambao wamejikuta wakivimba vichwa baada ya kupewa sifa za kijinga wakiambiwa kuwa filamu zao zinafanya vema katika tasnia hiyo.

Kwa nini nasema hivyo: sababu kubwa iliyonifanya nizungumze hivyo imechangiwa na hivi karibuni kwa baadhi yao na si wote kukataa ofa ya kupewa mafunzo ya fani hiyo bila ya kutotoa chochote kitu ofa ambayo ilitolewa na waandaazi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF).

Hali hii kwa tasnia ya filamu kwangu nadiriki kusema kuwa haiwezi kutufikisha popote na kuinua tasnia hiyo na kila siku tutabaki kutengeneza filamu ambazo zimekuwa haziongezeki ubunifu unaowezesha kupigisha hatua moja mbele.

ZIFF imeona kuna umuhimu wa kutoa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo watu wa tasnia hiyo kuwa wabunifu wa kimataifa hata pindi wanapoingia katika maonyesho hayo wawe na uhakika wa kufanya vizuri kama wasanii wengine walioendelea.

Katika hali ya kushangaza hakuna msanii hata mmoja ambaye alijitokeza kuchangamkia fursa hiyo adimu hali iliyosababisha hata waandaaji wasononeke.

Ofisa Mtendaji Mkuu anayemaliza muda wake, Profesa Martin Mhando, akizungumzia kuhusu hilo alinisononesha kwa kuwalalamikia Watanzania kutochangamkia mafunzo hayo maalumu ili kuongeza upeo wao na badala yake wengi wamebaki wakiishutumu ZIFF kwamba haiwasaidii kitu katika tasnia hiyo.

Mhando alisema kuwa: “Tunatumia gharama kubwa kuandaa mafunzo hayo na kuwaleta watu ambao unaweza kusema ndiyo sinema zenyewe, lakini unajikuta hakuna Mtanzania aliyeomba na badala yake unawapata watu kutoka nje mpaka Israel wakiuliza namna ya kufika na kuhudhuria,” alisema Prof. Mhando.

Katika tamasha la 14 la mwaka huu la ZIFF wamejitahidi kuandaa mafunzo mengi yakiwamo ya matumizi ya kamera HD, uandishi wa muongozo wa filamu, mambo ya muziki, uongozaji wa ‘dokumentari’ na utengenezaji wa filamu.

Pamoja na kusikitika kwa jinsi ambavyo wasanii wa Tanzania wanashindwa kutumia nafasi ya ZIFF kujiendeleza, Profesa Mhando alisema kwamba tamasha la mwaka huu limeendelea kuleta sura mpya katika tasnia ya sinema nchini.

Kwa hilo ningependa kuwaeleza wasanii wa nyumbani kutumia fursa hizo za bure.

Habari na Shabani Matutu

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.