04 Julai 2011

Mzuka Filamu za Kiswazi Wafifia ZIFF - Monalisa

Mzuka Filamu za Kiswazi Wafifia ZIFF - Monalisa

MAONYESHO ya Filamu za kiswahili yaliyopewa jina la Swahili Film Day katika tamasha la filamu la nchi za Majahazi (ZIFF) kwa mwaka huu yamekosa msisimko kulinga na mabadiliko ya ratiba tofauti na mwaka uliopita, Wadau wa filamu waliohudhuria tamasha hilo kwa mwaka huu wamesema mambo yamebadilika sana, na kama mwelekeo wenyewe ni huu mwaka ujao ni hatari.

Muigizaji na mtayarishaji wa Filamu ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya ZIFF kwa mwaka uliopita Yvonne Cherryl (Monalisa) anasema kuwa inawezekana moja ya sababu ya kukosa msisimko uenda ni kutokana na ratiba ilivyopangwa na kujikuta waalikwa wengi wakiwahi kuondoka na kurudi makwao na hata wale wenyeji wakikosa mwamko na maonesho hayo ambayo siku za nyuma yalikuwa maarufu sana.

“Niliondoka na kuingia Zenji siku ya Jumapili ambayo ndiyo siku iliyopangwa kuonyeshwa filamu za Bongo, katika siku maalum ya Swahili Day mambo ya Bongo Movie, lakini dah,, kwa mtu ambaye amekuwa akihudhuria tamasha hili kumetokea utofauti mkubwa sana kwani siku hii ya Jumapili ilikosa watu kabisa hali iliyopelekea kukosa msisimko kabisa, tatizo ni kutolewa kwa Awards siku moja kabla yaani Jumamosi, tofauti na ilivyozoeleka kuwa siku ya mwisho ndiyo tuzo hutolewa” Anasema Monalisa.

Anaendelea kusema kuwa wahusika wengi baada ya kugundua ni nani amechukua tuzo hawakujona sababu ya kuendelea kuwepo mahali pale wakati tayari walikuwa wanajua mshindi ni nani, hata hizo tuzo wengi wamezipokea kwa hisia tofauti kwa sababu mfumo nao wa utoajia tuzo hizo umewachanganya wadau wa filamu wa hapa nchini.