Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
05 Julai 2011

Wapemba Wapiga Hodi Soko la Filamu

Wapemba Wapiga Hodi Soko la Filamu

Kuna uwezekano mkubwa mara nyingi unaposikia neno "Pemba" picha inayokujia kwa haraka katika fahamu zako ni karafuu na marashi yake. Basi fahamu zako ziko sahihi kabisa lakini kuna zaidi ya hilo unaloambiwa na fahamu zako, Pemba kumeibuka wasanii wa tasnia ya filamu na wameingia kwa kishindo katika soko la tasnia hiyo.

Kutoka katika wavuti ya Filamu Central tunahabarishwa kwamba WASANII wa filamu kutoka Visiwa vya Pemba Zanzibar wamekuja na filamu inayokwenda kwa jina la Rupia. Katika filamu hiyo mtunzi anajaribu kuongelea hatari ya kukiuka maagizo kutoka kwa wazazi na wakubwa wao, pale Aboud Khalid anapomsaliti mkewe halali kwa kuuza Rupia mali aliyopewa na mkwewe, anaiuza bila kumshirikisha mkewe jambo linalomletea matatizo makubwa.

“Hii ni hadithi ya kweli na iliwahi kutokea siku za nyuma hapa hapa Pemba, kuna mtu ambaye alimsaliti mkewe kwa kudhulumu Rupia mali waliyokabidhiwa kutoka kwa baba wa Bi harusi ikiwa kama zawadi kwa ajili ya kumuoa mwanaye, na tumeamua kuitengeneza filamu hii kwa sababu ya mafunzo kwa jamii hasa jambo la uaminifu” Anasema Director wa Filamu hiyo Seif S. Said ( Seif Puche)
Lakini jambo la kuijvunia katika filamu hii ni kwamba wasanii wote walioigiza katika filamu hii ni kutoka katika Kisiwa hicho cha Pemba na wameonyesha uwezo wa hali ya juu katika kuigiza filamu hiyo yenye uhalisia, Filamu hii imetengenezwana na kampuni ya Kich Bwayz Vision (Kichungani Video Production)

Filamu hii ya Rupia hadithi ya kweli iliyotokea katika kijiji cha Kichungwani Chake chake Pembe imewakilishwa na Wasanii wenye vipaji ambao ni Aboud Khalid, Khadia Faki, Salum Madaira, Fatuma Mohamed, Othman Kondo, Mzee Fikirini na wengine wengi, filamu hii imeongozwa na Seif Puche akisaidiwa na Bi. Joha Sarahan, filamu hii itasambazwa na Whatever Film Produciton

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.