05 Julai 2011

Afande Bado Kakaza Ile Ile ya Mwaka

Afande Bado Kakaza Ile Ile ya Mwaka

Toka pande za Morogoro, Selemani Msindi 'Afande Sele' ameendelea na msimamo wake wa kutofanya kazi yoyote ya muziki kwasasa mpaka  pale ukiritimba utakapomalizika kwenye vyombo vya habari.

"Naendelea kusisitiza kuwa, ni bora nibaki kulima muhogo huku Morogoro kuliko kila siku kufanya kazi ambayo mwisho wake inakuwa ni kama hewa tu kwa kukwazwa na baadhi vyombo vya habari,” alisema Afande.

Alisema kuwa, wasanii wengi wamekuwa wakilipa pesa kwenye vyombo hivyo si kwa nia ya kutangaza nyimbo zao bali kutaka vibao vya baadhi ya wenzi wao wengine visisikike kabisa.

Habari na DHW