06 Julai 2011

Wolpa Aichana Filamu Central

Wolpa Aichana Filamu Central

MISEMO ya Wahenga Unena Ukweli unauma, lile sakata la wizi wa mkanda (Min Dv) wa Filamu ya God is Great kutoka Jijini Mbeya likiwa linaendelea na mhusika Jackline Wolper kujaribu kutetea hoja yake ya kuwa yeye hakuiba Dv hiyo bali alichukua kwa sababu alikuwa akiwadai watayarishaji walishindwa kumlipa ndio maana akaamua kumrubuni mpiga picha wa filamu hiyo na kuichukua kanda hiyo.

Siku ya jana muda wa saa mbili na nusu Jackline Wolper alimpigia simu mmoja wa wamiliki wa Mtandao huu na kuanza kummiminia matusi mfulilizo, eti habari za ukweli ambazo imekuwa ikiripoti kuhusu tukio hili la aibu kufanywa na mtu ambaye pia anajiita kuwa ni mtayarishaji wa filamu, anasema kuwa habari iliyomkera ni ile yenye kichwa cha habari “Kumbe Jack alikwapua Min Dv ili ajipatie Milioni 1 bila jasho”

“Hallow unajua naendesha gari ya Milioni Hamsini, Fenicha ya nyumbani kwangu ni milioni ishirini na tano, wewe Mayovela sijui Mwalovela, unajua mimi ni Super Star hujui nina uwezo kukufanya nini? Mnatafuta bifu wewe ulinipigia simu tukaongea, mimi siwezi kutaka milioni moja mimi nina hela, nitakufanyia jambo ambalo hautanisahau, alafu hajui wale jamaa wa Mbeya walichonifanyia, wale Ku…. , na wewe Ku…, zenu” Jackline Wolper akashusha mvua ya Matusi kama vile Rap mzuka umepanda.

Imekuwa si rahisi kuandika matusi kama alivyoyatamka yeye kwa sababu si maadili mema na pengine kama mimi nikiandika itaonekana kama mimi ndio natukana matusi hayo, mwanadada huyu baada ya ya kuwa analapu kwa vina vya matusi nilimweleza kuwa yeye kama anavyodai kuwa ni Star basi hastaili kuwa na tabia ya kukurupuka na kutukana matusi mfulilizo katika jambo lenye ukweli, hii ndio faidi ya kuandika habari za kweli.

Baada ya kutukana na kuridhika alimpigia simu mmoja kati ya wamiliki wa mtandao huu mwingine na kulalamika kuwa mtandao huu unalazimisha bifu na yeye Super Star na huku akitoa vitisho kwa mwandishi wa habari zake kuwa atamwonesha lakini kwa bahati nzuri alikiri kutukana akidai ni hasira, Uongozi wa mtandao huu unatafakari kuhusu tuhuma na matusi aliyotukana mwanadada huyu anayejita Super Star, lakini kuanzia sasa Picha nzima ya Uchafu uliofanyika Mbeya utaipata Live mpenzi wa FC.

Jack kama kweli wewe hauna tatizo wala shutuma za wizi wa Min Dv hii kwanini usiende Mahakamani ukawashitaki hawa Mbeya Film Production pamoja na hao wanaokuandika vibaya kuhusu sakata hili ikiwemo na FC ?
Lakini jambo lingine ambalo unatakiwa ukumbuke ni kwamba matusi uliyotukana tumerekodi na tunayo, ujumbe ambao umekuwa ukiwasiliana na wahusika tunao wote kama ushahidi, lakini si hivyo tu nakushauri nenda Mahamakani haki yako itapatikana kwa wale wote unaotangaza nao Bifu.

Jambo lingine taarifa ambazo FC inazo kuwa ulipewa ofa ya kusafishwa kashifa hii na kituo fulani ambao ni washikaji zako, lakini ulivyoambiwa uende kwa ajili ya mahojiano ulisema upo bize na kazi zako na ukamshawishi Amani amtafute Director wa filamu hii ya God is Great ili waende kukutetea na Amani alikwenda hadi Tabata Aroma kwa ajili ya zoezi hili lakini baada ya kuonana na Director huyu Herry G alikataa kuwa hawezi kufanya hivyo, swali linakuja kuwa kwanini haukutaka kwenda kujijitetea pamoja ukijua kuwa vituo hivi bosi ni mshikaji?

FC ina mambo mengi kuhusu wewe ambayo uliyafanya na mpambe wako Recho mkiwa Mbeya haya yamebaki kama ushahidi lakini ni lazima tutayaripoti, kwani hapo awali nikiambiwa kuhusu tabia yako ya kuwatukana watu na dharau sikuamini, lakini kwa hili kweli wewe hauna hizo sifa unazojipa kuwa wewe ni Super Star, na kama wewe ni Star kweli na Kanumba The Great, Ray, Irene Uwoya, na wengine tuwaite nani? Maana yeye hajiiti Super Star bali jamii inamwita The Super Star kupitia tasnia hii ya filamu.

Najaribu kukuelewesha kidogo maana haujitambui hata kidogo, The Great tunamwita Super Star kwa sababu Nyota yake inamrika hadi nchi ya Tanzania ndio maana hadi DSTV walimwita kama Nyota kwenda kupiga Stori na Washindani katika jumba la Big Brother Africa, hivi sasa jamaa ni balozi wa miradi kibao kwani basi usiwe wewe Jack mpenda sifa?

Kwa upande mwingine nawalaumu hata hawa Mbeya Film walikupa hadhi ambayo hauna katika tasnia ya filamu kwani kwangu mimi wewe hata katika kumi bora ya waigizaji wa kike haupo, ndio maana leo hii unawasumbua hadi wanashindwa kumalizia kazi yao kwa sababu ya wewe kuchukua kanda yao kwa madai ya Tshs. 400,000/= ambazo wao walikuwa tayari kukulipa lakini ukadai fidia ya Milioni 1 dada yangu wewe ni Mahakama hadi upange fidia ya kulipwa kesi ilifanyika katika Mahakama gani?

Nimeambiwa kuwa kuna una jamaa yako Mwanasheria ambaye huyu Recho amekuwa akiwanyanyasa hawa mabosi wenu wa Mbeya, kama kweli yupo basi mmeshindwa kumtumia vema katika kazi zenu, Jack FC ipo mbele yako kwa kila jambo unalofanya tunajua nyuma yako yupo nani lakini hawezi kujiigiza katika ujinga wako, ili ujue kuwa sisi tuna takwimu zako kwa kila hatua nakupa kidogo, jumatatu ulitakiwa kwenda kurekodi filamu Kibaha lakini haukwenda.

Haukwenda pamoja ulikuwa tayari umelipwa advance, na ulipopigiwa simu ukasema kuwa ulikuwa umempeleka mama yako Hospital wakati ulikuwa katika Hotel fulani na mtu fulani tunamheshimu hatuwezi kumtaja jina, lakini kama kweli Jack una fedha unazojinadi mbona wakati unarudi kutoka Mbeya ulikata tiketi ya daraja la chini wakati unaenda Mbeya uliwapa masharti mabosi zako wakukatie tiketi ya daraja la kwanza na wakafanya hivyo!!

FC haipo kwa ajili ya kumremba mtu bali kusema ukweli bila kuendekeza maigizo na kuwanadi wasanii kwa ajili ya uongo, unalotakiwa kujua ni kwamba FC ipo nawe hatua kwa hatua kwa kila jambo utakalofanya tutaripoti kwa usawa bila upendeleo.