06 Julai 2011

Fella Atumbukia kwenye Taarab

Fella Atumbukia kwenye Taarab

Unaweza usiamini lakini ukweli ni kwamba bosi mkuu wa kundi la 'TMK Wanaume Family' Said Fella, anaandika historia kwa kuamua kupanda jukwaani akishika ‘Mic’, ili kuinadi albamu yake ya muziki wa Taarab.hahaha

Fella ambaye anasema albam hiyo ambayo bado hajaipa jina,tayari amekwisha rekodi nyimbo 5  na anaanza rasmi kuinadi huku tayari akiwa ameshajipanga kuandaa maonyesho ambayo ataimba  akiwa na bendi yake mpya ya Mkubwa na Wanawe, aliyoianzisha hivi karibuni.

“Mkubwa kuanzia sasa nimeamua kushika mic na ninaanza kuimba kuzinadi nyimbo za albamu yangu ya taarab, nitaandaa maonyesho na pia nitashiriki kwenye maonyesho ya makundi mengine ya taarab na pia kama mtu atanihitaji katika onyesho lake, tutajadili mambo ya maslahi, nikiridhika nitaimba,” alisema Fella.

Katika albamu yake hiyo, Fella amewashirikisha wakali wa mipasho wakiwemo Hassan Kumbi, Maua Tego, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ na malkia wa mipasho nchini Khadija Omari Kopa.

Habari na DHW