Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
06 Julai 2011

Irene sasa Kutoka Kivyake Fulu

Irene sasa Kutoka Kivyake Fulu

MUIGIZAJI wa filamu mwenye jina kubwa katika tasnia hii Irene Uwoya anasema kwa sasa hatoshiriki kuigiza katika filamu ya Mtayarishaji mwingine zaidi ya Filamu zake ambazo atakuwa akitayarisha mwenyewe, sababu ya kufanya hivyo ni kujipa muda wa kutosha kwa ajili ya kufanya kazi zake, anaposhiriki filamu za watu wengine anajikuta akibanwa sana na muda na hana uwezo wa kumpangia muda mwenye filamu.

“Kwa sasa sitoweza kushiriki filamu za watu wengine zaidi ya filamu ambazo nitakuwa naziandaa mwenyewe, nafanya hivyo ili nipate muda wa kumlea Baby Krish na kutumia muda kwa ajili ya kupumzika zaidi ili kutengeneza filamu bora, lakini pia ukionekana sana watu wanakozoea unakuwa hauna mvuto kwao” Anasema Irene.

Irene ambaye kwa sasa yupo katika ulezi wa mtoto wake wa kiume Krish anasema kuwa yupo katika mazoezi ya kujifunza Lugha ili aweze kuigiza filamu katika nchi ya Cyprus ambako ndiyo makazi yake kwa sasa anakoishi na mumewe Hamad Ndikumana lakini kwa sasa wapo katika Likizo ya Uzazi hapa Tanzania nyumbani kwao, FC inamtakia maisha mema na mafanikio kwa ujio wa Baby.

Habari na FC

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.