Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
08 Julai 2011

Wabongo, DSTV - Swahili ni Kwa Ajili Yetu

Wabongo, DSTV - Swahili ni Kwa Ajili Yetu

WASANII wa fani mbalimbali hivi karibuni wamepata faraja ya kuwawezesha kutangaza fani zao kupitia kituo cha televisheni cha DSTV katika mpango unaojulikana kama AfricanMagic Swahili.

Katika uzinduzi huo wa chaneli hiyo ya Kiswahili walihudhuria wasanii pamoja huku wandishi wa habari nao hawakuachwa nyuma katika kuchukua tukio hilo la pekee kwa wasanii hao.

Chaneli inayopatikana kwenye Dstv mtandao namba 127 utaweza kuangaliwa na mamilioni ya watu wanaotumia lugha ya Kiswahili.

Kama inavyoaminika kuwa Kiswahili ni lugha adhimu, iliyofanikiwa kusambaa kwa haraka karibu duniani kote, hivyo ni wakati wa wasanii wetu kujiandaa kutoa kazi zenye ubora utakaoweza kulitangaza taifa.

Kwani mtandao huo utakuwa ukionyesha kazi za sanaa kama vile filamu, muziki wa kizazi kipya, hadithi na nyinginezo zilizoandaliwa kwa lugha hiyo adhimu.

Pamoja na kazi za wasanii wa Tanzania pia yapo mataifa mengine ya Afrika Mashariki ambapo hutumia lugha ya Kiswahili, watahusika na mpango huo.

Hivyo naamini kuwa kutokana na washiriki hao kutoka nchi hizo, kutakuwa na mashindano makubwa ya wasanii katika kujipmbanua kiubora.

Naamini kuwa wasanii wababaishaji hasa wale waliozoea kuiba ama kukopi kazi za wengine hawatakuwa na nafasi katika chaneli hii.

Kinachotakiwa kwa wasanii wetu ni kujipanga vizuri ili kutoa kazi ambazo zitaweza kutoa ushindani wa kweli na kuwatumbuiza waangaliaji wa chaneli hiyo ipasavyo.

Kazi hizo naweza kusema ni zile hasa zinazolenga maadili na utamaduni wa Kitanzania bila kuiga tamaduni za watu kutoka nje.

Hali hiyo itawawezesha watu wa mataifa mbalimbali kupata fursa ya kufahamu na kujifunza mambo mbalimbali yakiwamo yale ya vivutio vya kitalii hapa nchini na kwavutia kuja kutembelea vivutio hivyo.

Aidha, wasanii wetu wanapaswa kuwa makini katika suala la kuzipeleka kazi zao hizo, nikiwa na maana kwamba ni lazima waelewe watanufaika vipi na utaratibu huo.

Ni mpango mzuri wa kuwatangaza lakini hautakuwa na maana kama utakuwa hauna manufaa kama inavyojitokeza hivi sasa.

Hivi sasa wasanii wengi wamekuwa hawanufaiki na kazi zao ukilinganisha na wazalishaji ambao moja kwa moja wamekuwa chanzo cha hali ngumu ya kimapato kwa wasani hao.

Tutarajie kazi hii kubwa iliyofanywa na Multichoice ya kuwapatia wasanii wetu nafasi hiyo iwe mkombozi na itakayowaletea tija.

Haitapendeza kama mpango huo wa AfricanMagic Swahili utakwenda kinyume katika kusimamia maslahi ya wasanii, kitendo ambacho kinaweza kuwaondolea imani na hatimaye waonekane matepeli mbali ya wasanii.

Lakini sidhani kama MultiChoice wanaweza kuwaendea kinyume wasanii katika kusimamia haki zao.

Kama watafanya vizuri katika kuwainua wasanii kimaslahi kwanza wa kupata pongezi atakuwa ni Multichoice ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuwatafutia wasanii hao mafanikio.

Mtazamo wangu katika mpango huu, ninawashauri sana wasanii wetu waanze kubadili misimamo yao ya uandaaji wa kazi zao na wakubali kushauriwa katika kile ambacho kinawakera wadau wao.

Nimeamua kusema hivyo kutokana na ukweli kwamba wapo baadhi ya wasanii wetu hapa nchini wasiopenda ushauri japo wanachofanya katika jamii hakistahili.

Iwapo watakubali ushauri huenda safari yao hiyo na AfricanMagic Swahili ikawa ya mafanikio zaidi na kuwakwamua kimaisha.

Mwisho, tunarajia wasanii wetu wataandaa kazi zenye mvuto na zenye lugha isiyo na ukakasi kwa watazamaji wa chaneli hiyo, ambayo inafunguliwa saa 11:00 jioni na kuendelea kutoa burudani hadi saa 5:00 usiku kila siku, mpango ambao umekwishaanza tangu Julai mosi mwaka huu.

Habari na Shehe Semtawa

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.