Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
08 Julai 2011

Wasanii wa Kizazi Kipya Tumbukieni Filamuni

Wasanii wa Kizazi Kipya Tumbukieni Filamuni

KARIBUNI wapenzi wa sanaa ya filamu nchini katika kona hii ya Vunja vunja inayozungumzia masuala ya filamu za ndani.

Leo katika eneo hili nitakuwa nikiwaomba waimbaji wa muziki kujiingiza katika uigizaji wa filamu ili kujiongezea kipato na kupanua wigo wao wa sanaa.

Hivi karibuni kuliibuka kwa taarifa zilizokuwa zikihusisha makundi hasimu ya TMK Wanaume Family na TMK Wanaume Halisi waliouchukua uamuzi wa pamoja wa kutengeneza filamu ya pamoja itakayoelezea filamu inayohusu historia ya wasanii hao ambao walikuwa wakiunda kundi la kwanza kabla ya kuvunjika la TMK Wanaume Family.

Kona hii imepongeza uamuzi wa wasanii wa makundi hayo kuchukua hatua hiyo.

Kwa sababu wengi hawakuwahi kutarajia kama kuna hatua kama hiyo ingeweza kutokea kwa makundi hayo hasimu kukutana na kufikiria kufanya kazi pamoja ya filamu.

Nakumbuka wakati walipotangaza utengano baina yao makundi hayo yalikuwa na vita kali kutokana na kuwa na maskani zao jirani hali iliyosababisha kufikia kupambana kwa maneno na vitendo.

Katika mapambano yao mahasimu hao walifikia hatua ya kupelekana polisi na wengine kujikuta wakilazwa kituoni.

Mashabiki wengi wa makundi hayo ambayo wakati fulani yalifikia kutengeneza fedha kwa kupitia uhasama wao kwa kufanya tamasha la mashindano katika mikoa mbalimbali.

Taarifa hizo zilizungumzwa na mtengenezaji wa filamu hiyo, Hassan Umande, maarufu kama Chichi, aliyebainisha kuwa mpaka sasa wamefikia muafaka na kazi ya maandalizi ya filamu hiyo yanaendelea.

Kujitokeza kwa kundi hilo kufanya kazi ya filamu itakuwa imewafungulia njia wasanii wengine wa kuigiza kujitumbukiza katika uwanja wa tasnia hiyo ambayo kwa sasa ni gumzo hapa nchini.

Wasanii watakapojiingiza katika uigizaji watakuwa wamefanikiwa kwenda sambamba na wale wa Marekani ambao wengi wao wamekuwa wakijihusisha na uigizaji.

Kwa uamuzi wa Wanaume kuigiza filamu hiyo ya historia yao isiwe mwisho wao ila waendelee na kuigiza filamu nyingine.

Wasanii hawa watakuwa wameibua hisia za wapenzi wa muziki waliowahi kuiona filamu ya ‘Girl Friend’ iliyokuwa imekusanya nyota kibao wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la East Coast Team (ECT).

Pia wasanii wengine kama Jafarai na Banana zoro waliowahi kuonekana kwenye filamu ya ‘Siri’ wanaweza kushawishika kurejea katika tasnia hiyo ambayo wameipa kisogo.

Katika nchi zilizoendelea wasanii wakubwa wamekuwa wakionekana katika tasnia ya filamu kama vile 50 Cent, Eminem, Britney Spears, Willie Smith, Queen Latifa, JustinTimberlake na wengine wengi.

Hivyo kwa hapa nyumbani baada ya ufunguo wa Wanaume ningependa kutoa wito kwa wasanii wengine kufikiria kujikita kwenye tasnia ya filamu ili iweze kupata msisimko zaidi kuliko hapa ilipo.

Naamini wasanii kama TID, AY, MwanaFA, Dully Sykes, Bwana Misosi, Banza Stone, Ali Choki, Gurumo, Hassani Moshi na wengine kibao watarejea.

Habari na Shaban Matutu

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.