Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
10 Julai 2011

Tino Azipa Kisogo FIlamu za Mapenzi

Tino Azipa Kisogo FIlamu za Mapenzi

MSANII maarufu wa filamu nchini, Hissan Muya ‘Tino’, ameapa kutocheza tena filamu za kimapenzi badala yake atacheza filamu za mapigano zinazoelimisha jamii.

Akizungumza hivi karibuni Tino alisema kuwa kwa sasa amesitisha mpango wa kutengeneza na kucheza filamu za mapenzi kwa kuwa wengi wamejikita kutengeneza filamu za aina hiyo na kusahau mambo muhimu yanayoigusa jamii hasa janga kubwa la ukimwi, njaa na mengine mengi.

Tino alisema sababu nyingine ya kuzitosa filamu za mapenzi ni baada ya kutengeneza filamu ya ‘Shoga’ na baadaye kubadilishwa jina na kuitwa ‘Shoga yangu’ iliyokuwa na lengo la kuelimisha jamii kuhusu suala zima la ushoga, badala yake ijana kumletea matatizo.

“Sitaki kucheza tena filamu za mapenzi, sasa hivi nataka kugeukia kwenye filamu za mapigano na zile zinazogusa maisha ya binadamu wa kawaida,” alisema Tino.

Tino ambaye kwa sasa anatesa na filamu yake mpya ya ‘Shoga yangu’ ambayo ipo sokoni, amewashauri wasanii wengine kutojikita sana katika filamu za mapenzi, ambapo alisema kuna stori nyingi zikiwemo zile za Watanzania wanaopatwa na majanga mbalimbali hapa nchini.

na Samia Mussa

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.