Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
10 Julai 2011

Wasanii Mnatambua Juhudi za Serikali?

Wasanii Mnatambua Juhudi za Serikali?

MIEZI mitatu iliyopita serikali imeonyesha mwelekeo wa kutaka kuisaidia nyanja ya sanaa na utamaduni baada ya kelele lukuki kutawala nyanja hizo muhimu hapa nchini.

Sababu zilizoonekana kuwa kikwazo katika nyanja hizo kwa upande mwingine zinaonekana ni kutokujitambua kwa wasanii ambao wanapiga kelele kila siku.

Mara zote wasanii wanapiga kelele kutokufanikiwa kwa kazi zao na maendeleo yao hali ambayo mwisho wao haulingani na kazi walizofanya.

Lakini inatia uchungu kwa wasanii waliofanya makubwa katika tasnia hizo na kufikia mwisho ambao ukielezwa kwamba ndiye aliyewahi kutenda jambo fulani, havifanani!

Pamoja na matatizo hayo, serikali nayo ilionyesha kuikimbia tasnia hiyo adhimu ambayo kwa nchi zilizoendelea inachukua nafasi kubwa ya pato la taifa. Mfano, kwa nchi ya Marekani.

Inaonyesha kwamba kutokuwa na mpangilio bora kwa wasanii ndicho kikwazo ambacho kimesababisha serikali kuikacha tasnia hiyo.

Mwaka huu, serikali imeona umuhimu wa tasnia za sanaa na burudani kwamba ni mojawapo ya tasnia ambazo zikiwezeshwa zitaleta pato kubwa zaidi kwa serikali kwa ujumla na si kama inavyodhaniwa.

Tanzania Daima ni taasisi ambayo inafanya kazi na jamii, inapongeza hatua ya serikali kwa kutambua kwamba sanaa na utamaduni vinaweza kuchangia sehemu kubwa ya pato la taifa.

Ushawishi uliosababisha serikali kufikia hatua hiyo ni ambao ulifanywa na mwanauchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Jehovaness Aikael, ambaye alitoa tathmini ya pato la taifa kwa miaka mitano iliyopita, akasema lilikuwa ni shilingi bilioni 71, tena kwenye tasnia ya muziki pekee.

Inaonyesha kwamba serikali hadi iamshwe kwa takwimu kama iliyotolewa na mwanazuoni huyo ni sehemu mojawapo ya hatua ambazo zimeishtua serikali kwa kiasi fulani.

Pamoja na kwamba serikali imeanza kuonyesha mwelekeo wa kujali tasnia hizo, lakini wasanii nao wajipange kwa ajili ya mapokeo hayo kutoka serikalini.

Wasanii wanatakiwa waonyeshe kuipokea serikali kwa vitendo, hasa kuandaa masuala kama kumbukumbu na upangaji wa bei za bidhaa zao na si kila mmoja kufanyabiashara peke yake.

Kinachorudisha nyuma maendeleo ni pamoja na kutokuwa na msimamo kwa wasanii, hasa kwa uuzaji wa kazi zao.

Wakiweza kufanikisha hatua hizo, hata ushindani wa soko la Afrika Mashariki ulioanza Tanzania itafanikiwa ipasavyo badala ya kila msanii kufanya kazi peke yake, jambo ambalo badala ya kwenda mbele tunarejea tulikotoka.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.