10 Julai 2011

Bado Nipo Nipo Sanaaa - Lulu

Bado Nipo Nipo Sanaaa - Lulu

Azidi kufunnguka sasa kwenye chati za filamu za kibongo hapa nchini, huku akiwaweka watu vinywa wazi baada ya kusema kule kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa 'Bado nipo nipo Sanaaa'.

Si mwingine bali ni yule msanii wa filamu za kibongo Elizabeth Michael 'Lulu', kwa sasa anakuwa sahani moja na nyota wa hapa Bongo.

Kutokana na uzuri wa mwanadada huyo huku akipambana na changamoto za hapa na pale zikiwemo 'skendo' zisizoisha juu yake, aliweza kukitingisha kibiriti kama kimejaa baada ya hapo awali kudaiwa kuvishwa pete na jamaa fulani kitu ambacho siyo cha ukweli.

Lulu ni msanii pekee aliyeanza sanaa toka akiwa na umri mdogo kwenye kundi la Kaole Sanaa Group, ambalo ndilo lililozalisha mastaa mastaa wa Bongo akiwamo Ray Kigosi pamoja na Steven Kanumba.

Habari na DHW