Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
10 Julai 2011

Afadhali Filamu Kuliko Tamthilia - Nkwabi

Afadhali Filamu Kuliko Tamthilia - Nkwabi

MUIGIZAJI Nyota anayetamba katika tamthilia ya 69 Records inayorushwa na kituo cha Clouds Tv Juma A. Nkwabi anasema kwa katika uigizaji wa filamu ni rahisi kuliko Tamthilia iwapo tamthilia hiyo itakuwa imepangiliwa kwa kufuata taratibu husika, akiongea na FC amesema kuwa pamoja na kuigiza katika tamthilia inayoendelea lakini kabla ya kuingia huko alikuwa katika uigizaji wa Filamu.

“Kwangu mimi naona kuigiza filamu ni jambo rahisi sana, hasa pale tamthilia unayoigiza itakuwa imefuata taratibu za uandaji wa tamthilia hiyo kitaalamu, lakini ukija katika filamu si kazi sana kwani hata kushika script haichukui muda mrefu kama ilivyo katika tamthilia, lakini unapoigiza tamthilia kwa hapo nyumbani inakuwa kazi ngumu zaidi kulingana na waandaaji wetu” Anasema Nkwabi.

Aidha anaeleza kwamba katika filamu zote ambazo ameigiza anaipenda sana filamu ya 007 kwani pamoja na kuigiza katika filamun kibao lakini hakujulikana lakini alipoigiza katika filamu hii kila mtu alitambua kuwa Nkwabi yupo katika waigizaji bora na makini na kila mtayarishaji alianza kumtafuta kwa ajili ya kushiriki katika filamu ambayo anatayarisha, Nkwabi kashiriki filamu kama wrong number, Brothers, Tafrani na filamu nyinginezo.

Hivi sasa Nkwabi yupo mbioni kutoa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Dimbwi la Mapenzi ambayo katika filamu hiyo amemshirikisha msanii mwingine katika fani hiyo Steve Sandhu.

FC

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.