Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
11 Julai 2011

Ray Njiani na Vikali Vipya

Ray Njiani na Vikali Vipya

MUONGAZAJI na muigizaji nyota katika tasnia ya filamu hapa nchini Vicent Kigosi (Ray The Greatest) kupitia kampuni ya RJ Company ametambulisha vipaji vipya katika filamu zake mbili kali za Unpredictable na What is it?, kampuni hii mahiri katika kuibua vipaji na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya tasnia hii ya filamu nchini, inawaleta wasanii wawili wapya kabisa ambao ni Irene Paul na Otilia Joseph.

Akiongea na FC mmoja kati ya Wakurugenzi wa kampuni ya RJ Blandina Chagula aka Johari ameeleza kuwa kampuni yao inaibua vipaji vipya pamoja na kuvitoa kupitia kazi ambazo zinazalishwa na kampuni hii ya utengenezaji wa filamu mahiri kwa hapa nchini, ujio wa safari hii kampuni inamtambulisha Irene na Otilia.

“Tunatarajia wapenzi wa filamu Tanzania na nchi ambazo wanapenda filamu za Kitanzania kuona vipaji vipya Irene na Otilia, kutoka RJ Company wakija kwao na kazi nzuri, ambazo ni What is it? na Unpredictable, wasanii hawa wameonyesha uwezo wa hali ya juu chini ya Muongozaji mahiri wa filamu kutoka RJ Ray The Greatest” Anasema Johari.

Pia kampuni hii inatarajia kuendelea kuwatambulisha wasanii wengine wenye vipaji ambao wanasifa na vigezo bora watakao kuwakichaguliwa katika utaratibu uliwekwa na kampuni hii, FC inatoa pongezi kwa kampuni hii kuwa chachu ya mabadiliko ya tasnia hii ya filamu Tanzania.

Habari na FC

1 maoni

  • Maoni Winston 11 Julai 2011 Winston

    Hiyo safi, ila usiishe kuwamega tu, uwatoe kwelikweli maana nyie maprodyusa wa Kibongo tunawajua tabia zenu

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.