Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
12 Julai 2011

Home Village 2 Njiani

Home Village 2 Njiani

SEHEMU ya pili ya filamu kali na ya kusisimua ya Home Village ipo tayari na inategemea kuingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa, filamu hii katika sehemu ya pili watengenezaji wametumia utalaam wa Teknorojia ya kisasa kabisa ambayo inawezekana ikawa ndiyo filamu ya kwanza kutumika katika filamu ambazo zimetengenezwa na kuingia sokoni katika tasnia ya filamu kwa hapa nchini.

“Baada ya sehemu ya kwanza kupokelewa kwa shangwe na wapenzi wa filamu kwangu imenipa changamoto zaidi katika kuongeza ujuzi zaidi kwani ni jambo linalohitaji ujuzi na maarifa katika kutengeneza kitu kizuri kupita cha kwanza hii inakuwa ni maendeleo na mimi nimeliona hilo na kulifanyia kazi katika levo za juu zaidi” Anasema Tico.

Aidha mtaalamu huyu ambaye ndiye aliyehariri filamu hii anasema kuwa Home Village ni filamu ambayo muda mwingi anaumiza kichwa kwa ajili ya kuifanya iwe tofauti kabisa na kazi ambazo tayari amezifanya, kwa mantiki hiyo anajikuta muda mwingi analazimika kuwasiliana na watu wake walio nje ya nchi kwa ajili ya kuibororesha na kuwa kitu tofauti na cha kisasa huku lengo likiwa kuingia katika soko la Kimataifa.

Home Village inakutanisha vichwa kibao vikali huku mbele yao kukiwa na makamanda wao,yaani Jackson Kabirigi aka Bob Jack Mzee wa Tabu na mateso, Dady Ramadhan (Dady) kutoka Afrika ya Kusini, Denis David, Omary Clayton (Director Ommy), Ramadhan Sungura, Latifa Idabu (Badra) na wasanii wengine wakali katika tasnia hii ya filamu nchini.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.