Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
13 Julai 2011

Tamasha la Jivunie Utanzania Njiani - Kili

Tamasha la Jivunie Utanzania Njiani - Kili

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager imeandaa tamasha linalojulikana kama ‘Kilimanjaro Premium Lager Fun Festival’.

Kwa mujibu wa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, huo ni uzinduzi wa Kampeni ya Kili ‘Jivunie Utanzania’ kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.

Kavishe alisema tamasha hilo pia linalenga kuwaleta pamoja mashabiki wa Simba na Yanga, watakaopata fursa ya kucheza mechi tofauti, ambako washindi watapata zawadi mbalimbali zinazotolewa kwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager.

Simba na Yanga, ndizo klabu vigogo zaidi hapa nchini, ambazo pia hudhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

Kavishe alisema, tamasha hilo litafanyika viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar es Salaam Jumamosi, Julai 16 na ni kwa ajili ya umma wote.

“Hili ni tamasha la mashabiki linalolenga kutangaza zaidi kampeni yetu ya Jivunie Utanzania’ tuliyozindua kwa waandishi wa habari hivi karibuni kwenye Makumbusho ya Taifa,” alisema Kavishe na kuongeza kwamba, ushiriki wa kwenye michezo utakuwa wa hiari.

“Zitatolewa zawadi nyingi wakati wa tamasha hili, ambalo litakwenda sambamba na ‘carnival’ ambayo ni aina ya sherehe itakayofanyika barabara nzima kuelekea viwanja vya Posta, ili kuwahamasisha Watanzania kujivunia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru,” alisema Kavishe.

Aliongeza kuwa tamasha hilo linatarajiwa kuanza mchana na kumalizika jioni, ambako kutakuwa na bia za kutosha za Kilimanjaro na nyama choma ikienda sambamba nazo.

TBL kupitia Kampeni ya ‘Jivunie Utanzania’, imeandaa shughuli mbalimbali zitakazoendelea hadi Desemba, wakati wa kilele cha sherehe za Uhuru.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.