Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
17 Julai 2011

Kanumba Kulikoni na Mchumba wa Mtu?

Kanumba Kulikoni na Mchumba wa Mtu?

STAA wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba ‘The Great’ (pichani), amezua mjadala vichwani mwa wadau wa burudani ndani ya Ukumbi wa Bilicanas Posta, Dar es Salaam baada ya kunaswa usiku wa manane akiwa na mrembo aliyedai kuwa ni mchumba wa mtu ambaye jina halikupatikana.

Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu, Kanumba alikuwa ‘bize’ na kimwana huyo kiasi cha kuonekana walikuwa na uhusiano zaidi ya kuwa mtu na shemejiye wakati Bendi ya African Stars international ‘Twanga Pepeta’ ikiporomosha burudani ukumbini humo.

Wawili hao walikuwa wakichombezana kwa utundu huku vicheko na tabasamu vikichukua nafasi kiasi cha wadau wa burudani kuhisi kuwa wawili hao wana la ziada.

Awali, paparazi wetu alimshuhudia Kanumba akifika ukumbini humo saa 7:09 usiku, akiwa ameongozana na baadhi ya rafiki zake na kwenda kuketi kwenye kona moja iliyopachikwa jina la Bongo Movie.

Akiwa pande hizo, staa huyo aliagiza vinywaji na baadaye kucheza muziki na marafiki zake. Baada ya muda akatokea dada huyo na kuwa naye sambamba.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mapozi ya wawili hao yalizidi kuzua utata hasa kwa kimwana huyo kujisahau kama wako mbele ya kadamnasi na kupitisha mikono yake katika maungo ya Kanumba.

Baada ya kuona mapozi yamezidi, paparazi wetu alimfuata Kanumba na kumuuliza kuhusiana na ukaribu wake na msichana huyo.

“Aaah! Huyu ni rafiki yangu lakini  tena ni mchumba wa mtu, sioni ubaya kufurahia naye hapa ukumbini na mapozi yote haya ni kuonesha furaha tuliyonayo,” alisema Kanumba.

Hata hivyo, paparazi wetu alimtaka Kanumba afunguke kama kimwana huyo ni mbadala wa mchumba’ke waliyemwagana, Miss Ilala 2009, Sylvia Shally.

“Mmmh! Siwezi kuweka wazi sana lakini kama unavyoona, tunapeana kampani tu,” alichezesha  taya huku akipiga hatua kumpotezea ‘vuvuzela’ wetu.

Baadaye kila mmoaja alichukua hamsini zake.

2 maoni

  • Maoni Majotrooo 18 Julai 2011 Majotrooo

    Bora asioe kwanza maana kama ataoa halafu aendeleze mchezo huu ndo atakuwa kwenye wakati mgumu zaidi, watu wa dini nao watampa kibano kilekile cha mwaka. Isitoshe huyu jamaa yuko kwenye tasnia yenye mitego mingi kweli kweli, si unaona anavyotegwa hapo kwenye picha?

  • Maoni Bajabir 17 Julai 2011 Bajabir

    Mh,kanumbaaaaaa......this is tooo much,unawaaibisha hata wazaz wako,,,,,,,,oa sasa,maana wanawake ushawatumia vya kutosha sasa......

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.