17 Julai 2011

Kanumba Kulikoni na Mchumba wa Mtu?

Kanumba Kulikoni na Mchumba wa Mtu?

STAA wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba ‘The Great’ (pichani), amezua mjadala vichwani mwa wadau wa burudani ndani ya Ukumbi wa Bilicanas Posta, Dar es Salaam baada ya kunaswa usiku wa manane akiwa na mrembo aliyedai kuwa ni mchumba wa mtu ambaye jina halikupatikana.

Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu, Kanumba alikuwa ‘bize’ na kimwana huyo kiasi cha kuonekana walikuwa na uhusiano zaidi ya kuwa mtu na shemejiye wakati Bendi ya African Stars international ‘Twanga Pepeta’ ikiporomosha burudani ukumbini humo.

Wawili hao walikuwa wakichombezana kwa utundu huku vicheko na tabasamu vikichukua nafasi kiasi cha wadau wa burudani kuhisi kuwa wawili hao wana la ziada.

Awali, paparazi wetu alimshuhudia Kanumba akifika ukumbini humo saa 7:09 usiku, akiwa ameongozana na baadhi ya rafiki zake na kwenda kuketi kwenye kona moja iliyopachikwa jina la Bongo Movie.

Akiwa pande hizo, staa huyo aliagiza vinywaji na baadaye kucheza muziki na marafiki zake. Baada ya muda akatokea dada huyo na kuwa naye sambamba.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mapozi ya wawili hao yalizidi kuzua utata hasa kwa kimwana huyo kujisahau kama wako mbele ya kadamnasi na kupitisha mikono yake katika maungo ya Kanumba.

Baada ya kuona mapozi yamezidi, paparazi wetu alimfuata Kanumba na kumuuliza kuhusiana na ukaribu wake na msichana huyo.

“Aaah! Huyu ni rafiki yangu lakini  tena ni mchumba wa mtu, sioni ubaya kufurahia naye hapa ukumbini na mapozi yote haya ni kuonesha furaha tuliyonayo,” alisema Kanumba.

Hata hivyo, paparazi wetu alimtaka Kanumba afunguke kama kimwana huyo ni mbadala wa mchumba’ke waliyemwagana, Miss Ilala 2009, Sylvia Shally.

“Mmmh! Siwezi kuweka wazi sana lakini kama unavyoona, tunapeana kampani tu,” alichezesha  taya huku akipiga hatua kumpotezea ‘vuvuzela’ wetu.

Baadaye kila mmoaja alichukua hamsini zake.