Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
18 Julai 2011

Baada ya Kiba Sasa ni Mwasiti, Barnaba na Usher Raymond

Baada ya Kiba Sasa ni Mwasiti, Barnaba na Usher Raymond

BAADHI ya wasanii nyota kutoka kituo cha Tanzania House of Talents (THT), wamealikwa na msanii nyota nchini Marekani, Usher Raymond, kupitia taasisi yake ya New Look Foundation iliyoko jijini Atlanta.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, ziliwataja wasanii hao kuwa ni Mwasiti Almas, Amin Mwinimkuu, Barnaba, Ditto, Linah pamoja na mpiga kinanda, Mose Delema.

Nyota hao ambao wataambatana na mwanzilishi wa THT, Ruge Mutahaba, pamoja na mtangazaji wa kituo cha 88.4 Clouds Fm, Hamis Mandi ‘B 12’ wakiwa huko watapata nafasi ya kutumbuiza jukwaa moja na Raymond.

Aidha, wasanii hao pia watahudhuria katika mkutano wa kimataifa wa viongozi wa siku nne, pamoja na utoaji tuzo.

Usher, amewaalika nyota hao kuhudhuria mkutano huo utakaojadili mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kubadilishana ujuzi.

na Dina Ismail

1 maoni

  • Maoni Mzuks 18 Julai 2011 Mzuks

    Inapendeza kuona wasanii wetu wakizidi kukua, bonge la step sio kila siku muziki na umaarufu wako unaishi mtaani kwako pekee.

    Ila natoa rai hapa, wasanii wa Kibongo ongezeni kasi ya kupiga muziki wenu live, mambo ya playback na CD imepitwa na time.

    Mzuks

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.