Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
18 Julai 2011

Inspekta, Tundaman Kinomanoma Mbeya

Inspekta, Tundaman Kinomanoma Mbeya

Mastaa wa Bongo Fleva, Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ (pichani) na Khaled Ramadhan ‘Tundaman’ nusu watoane roho, Risasi Jumamosi linashuka nayo.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilijiri ndani ya Hoteli ya Mount Stone jijini  Mbeya ambapo jamaa hao walikuwa pande hizo kwa ajili ya Tamasha la Fiesta mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika tukio hilo, Inspector alishuhudiwa akimvaa Tundaman na kummwagia mvua ya maneno ‘mbofumbofu’ yasiyoandikika gazetini kwa madai kwamba anaringa huku akiwapotezea wakongwe wa gemu la muziki Bongo.

Awali, Tundaman alipiga kimya lakini Inspector aliendelea kumchana kuwa ana dharau kupita maelezo na ishu hiyo haikuanzia hotelini hapo kwani amekuwa akimfuatilia kitambo.

Baada ya kuona jamaa hatulii, Tundaman naye alikuja juu na kumchana Inspector kupita maelezo hivyo kuibua timbwili la aina yake hadi msanii Raheem Rumy Nanji ‘Bob Junior’ alipoingilia kati na kuweka mambo sawa.

Risasi Jumamosi lilipotaka kujua kulikoni na nini mustakabali wao, hakuna aliyekuwa tayari kufafanua chochote kutokana na kila mmoja kuwa na hasira.

http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/inspector-tundaman-nusu

1 maoni

  • Maoni lufinyo 18 Julai 2011 lufinyo

    Hivi Inspector baada ya zile rap katuni zake mbili alizotoa ameshafanya kazi gani nyingine iliyowahi kubamba?

    Nadhani jamaa kashaona he's out of the game kwa hiyo anatumia nguvu ya ziada kujibakiza kwenye magazeti.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.