Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
18 Julai 2011

Kazi Zetu Zimeibwa vya Kutosha - Wasanii

Kazi Zetu Zimeibwa vya Kutosha - Wasanii

MARA nyingi kama si mara zote, Tanzania imegubikwa na kelele ya wasanii wa nyanja mbalimbali kwa sababu ya kuibiwa na kudhulumiwa kazi zao.

Sanaa ni nyanja tanzu ambayo ikitumika ipasavyo, Tanzania itakuwa zaidi ya nchi zilizoendelea kuliko ilivyo sasa, kelele zimekuwa nyingi badala ya kujipanga na maendeleo yanayotafutwa kila leo.

Ifikie mahali wasanii wa Tanzania, wajione wana dhima kubwa kwa jamii, kwani wao ni sehemu ya elimu, kuburudisha na kukosoa, sauti zao zinafika mbali zaidi ya nyanja nyingine.

Wasanii wenyewe wakijipanga vilivyo, njia itakuwa nyeupe kuelekea kwenye mafanikio kama walivyo kwenye nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza.

Tanzania Daima ni taasisi ambayo inashirikiana vilivyo na taasisi na wadau mbalimbali, inawakumbusha wadau wa sanaa na wasanii kujitambua kwa sababu nyanja yao ni adhimu kati ya nyanja zote katika maendeleo ya jamii.

Kuna baadhi ya wasanii hawafahamu hata Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Chama cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA) na maeneo mengine ambayo wanatakiwa kushirikiana nayo katika kazi zao.

Kwa sababu, hivi sasa Tanzania inatakiwa kujipanga kwa ajili ya soko la Afrika Mashariki linalotarajia kufanyika hivi karibuni baada ya milango kufunguliwa, wasanii wetu hawapaswi kuendelea kushangaa.

Wenzetu wa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wamejipanga vilivyo kwa ajili ya soko hilo, lakini Tanzania, kila leo tunalia vilio visivyokwisha badala ya kusaka dawa ya maendeleo.

Ifikie mahali tutazame tulikotoka; miaka iliyopita wasanii wa Tanzania walikuwa wanalia kuhusu kudhulumiwa na kuibiwa kazi zao na wezi ambao dawa zake zinafahamika na zinaweza kufanyiwa kazi pasi na kupiga kelele.

Ili kufanya vizuri kwenye soko la pamoja la Afrika ni kujiandaa ipasavyo na ushindani wa nchi za Afrika Mashariki kuliko kulia kila uchao.

Na njia pekee ni kujitambua kwa wasanii kuliko wengine kupenda kuweka wazi masuala yao ya siri hadharani badala ya kuyaficha.

Tena cha kushangaza wengine wakishakamilisha kazi zao, wanakuwa na njaa ya ajabu; badala ya kuhimili njaa wanaziuza kwa gharama bei ya kutupa.

Ni wakati muafaka kwa wasanii wetu kujipanga vilivyo kwa ajili ya ushindani kuliko kusubiri majirani zetu kufanya vizuri katika soko hilo na kuanza kulia na kulalamika.

1 maoni

  • Maoni Khadija 18 Julai 2011 Khadija

    Kwa kiasi kikubwa wasanii mnajiibia wenyewe. Kukomesha wizi wa kazi zenu shuruti kila mmoja awe mlinzi wa kazi yake mwenyewe na pia awe mlinzi wa kazi ya mwenzake. Kwa mfano, kama unakwenda sokoni na kukuta kazi yako ikiuzwa visivyo piga kelele, ukiona kazi ya mwenzako inauzwa visivyo piga kelele watu wakamate mwizi.

    KWa mtindo huu wa kulinda na kulindiana mtapiga hatua kubwa sana katika kupunguza na si kuzuia wizi huu maana teknolojia inakwenda kasi sana kati kufanikisha wizi. Na ni lazima mkaelewa pia kwamba wizi hauko Tanzania tu, ni dunia nzima.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.