Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
19 Julai 2011

Mapacha Watatu Bega kwa Bega na Extra Bongo

Mapacha Watatu Bega kwa Bega na Extra Bongo

BENDI ya Mapacha Watatu juzi iliungana na Extra Bongo ‘Next Level’ kushambulia kwa shoo ya aina yake iliyofanyika ukumbi wa Zonghwaa Victoria jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wapenzi na mashabiki wa burudani katika ukumbi huo, mmoja wa wanamuziki wa Mapacha Watatu, Kalala Junior, alisema wao na Extra Bongo ni kitu kimoja, kwani wako katika ari moja ya kuendeleza, kukuza na kuleta ushindani katika medani ya muziki wa dansi.

“Tunamheshimu sana kaka yetu, Ally Choki, kama mkurugenzi wa Extra Bongo na tutaendelea kumheshimu na kumpenda, ikiwa ni kama kaka yetu katika muziki na ndiye aliyetuonyesha njia ya kujitambua na kujitegemea katika muziki wa dansi,” alisema Kalala Jr.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki, alishukuru kwa maneno mazuri kutoka kwa Kalala na kuahidi kuwaunga mkono katika kuiendeleza Mapacha Watatu, ingawa mwanzo mgumu, lakini watafanikiwa.

Extra Bongo na Mapacha walipiga kwa pamoja katika ukumbi huo na kukonga nyoyo kwa kukumbushia nyimbo za zamani ambazo walipiga pamoja enzi za nyuma wakiwa pamoja.

na Francis Dande

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.