Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
14 Machi 2011

Bongo Flava + Mipasho = Bab'kubwa

Bab'Kubwa

KUANZIA mwaka 1997 kurudi nyuma, mipasho haikuwa na thamani kubwa kama ilivyo hivi sasa kutokana na kasumba kuwa, muziki huo umekaa kike zaidi.

Wanaume wote waliokuwa wakiushabikia muziki huo walikuwa wakipewa majina yasiyofaa, haya na yale huku wengi wao wakihisiwa kuwa ‘hawafai’.

Lakini mambo yakaja kubadilika baadaye, kuanzia mwaka 1998, kwa baadhi ya vituo vya redio hasa 88.4 Clouds FM huku mtangazaji wake akiwa marehemu Amina Chifupa ‘AC’ kuwa mahiri katika kurindimisha vibao vya muziki wa aina hiyo.

Baadhi ya vya mwanzo kabisa kupigwa redioni ni pamoja na kile cha kundi la Tanzania One Theatre (TOT), kinachokwenda kwa jina la ‘Mambo Iko Huku’.

Kibao hiki kilitungwa na Kapteni mstaafu na Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba na kuimbwa na Malkia wa mipasho barani Afrika, Khadija Kopa.

Kutoka kibao hicho, kikafuatia kile cha ‘Hakuna Tenda, Hakuna Buzi ‘Paparazzi’, kilichopakuliwa na wakongwe wa miondoko ya mipasho, East African Melody Modern Taarab na kuimbwa na Bi Mwanahawa Ally.

Hata hivyo, redio hizo zilizoanza kupiga vibao vya mipasho wakati huo, zilikuwa zikidhihakiwa na redio pamoja na vyombo vingine vya habari kuwa ‘wote ndio haohao’.

Mabadiliko ya sera za habari na uhuru wa vyombo husika na mwamko wa Watanzania, viliposhika kasi, navyo vikaanza kuchangia kutokomea kwa kasumba ya kuwa mipasho ni muziki wa kike zaidi.

Kwani hivi sasa, mipasho ndiyo muziki unaoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi, ambapo umekamata vyombo vyote vya habari; redio, magazeti na televisheni zote nchini.

Kwa upande wa mashabiki, mipasho imefanikiwa kupora wanazi kutoka katika fani zote za muziki hapa nchini, ambapo si ajabu hata kidogo kuhudhuria tamasha la mipasho na kukuta viongozi wa kitaifa wakiserebuka.

Hivi karibuni, Meneja wa kundi la miondoko ya Bongo Fleva, Said Fella alionyesha kuiunga mkono mipasho kwa kutangaza onyesho la pamoja kati yao na mabingwa wa muziki huo, Jahazi Modern Taarab.

Nilipozungumza naye jana, jijini Dar es Salaam Fella anasema, ameamua kuandaa onyesho hilo la pamoja ili kuudhihirishia umma kuwa wasanii wake wanaisapoti vilivyo mipasho.

Fella anasema, onyesho hilo alilolisifu kwa kudai litakuwa la aina yake, limepangwa kurindima Machi 15, kwenye ukumbi wa Bulyaga, Temeke jijini Dar es Salaam.

Anasema wameamua kuliita onyesho hilo kuwa ni la ‘Usiku wa Mkono Mmoja Nyumbani TMK’ ambako watatambulisha kibao kipya cha Stiko na Kr kiitwacho ‘Chemka Nami’.

Binafsi nikiwa mdau nambari moja wa muziki na burudani kwa ujumla, nafurahishwa na hili na kuona kuwa mipasho, muziki usio na dosari, umefika mahala pazuri.

Hii ni kwa sababu, mipasho ndiyo muziki mkongwe ulioingia barani Afrika kwa kishindo katika miaka ya 1800, huku ukiendelea kutikisa hadi sasa.

Tayari tulishashuhudia matamasha kibao ya dansi na mipasho, ambapo sasa tumebakiza kushuhudia labda ya mipasho na muziki wa kunesanesa, reggae.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.