Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
20 Julai 2011

Elimu Ndogo Inaua Komedi - Mboto

Elimu Ndogo Inaua Komedi - Mboto

MCHEKESHAJI Mahiri wa Vichekesho Haji Salum almaarufu kama Mboto ameiambia FC kuwa moja kati ya matatizo yanayowakabiri wasanii wa Komedi ni ukosefu wa Elimu ya darasani na Mtaani pia, akielezea kwa undani Msanii anasema kuwa pamoja na kuwa wao ndio wanaohitajika na jamii lakini bado wamekuwa wakionekana kama vile ni watu wasio na umuhimu katika tasnia hii.

Tofauti na Wasanii wanaoigiza filamu ambao tayari kidogo wanaweza kujenga thamani ya kazi yao na kuweza kuthaminiwa na jamii kwa sababu tayari wao wanajitambua, mara nyingi baadhi ya Wachekeshaji wanashindwa hata kubadilika na kuonesha nia hasa ya kubororesha malipo kutoka kwa Watayarishaji wa kazi hizi, Mavazi ni hovyo hata maeneo nayo hayaridhishi.

“Unajua ikosefu wa Elimu kwa Makomediani wengi ni tatizo, kwani ukifuatilia sana utagundua kuwa wengi wao ni Darasa la saba lakini hilo hilo tulikuwa tunatega Mzinga, kwa hiyo hata kujenga umoja kwa ajili ya maslahi yetu inakuwa tabu, mimi na mwezangu tulianzisha Chama chetu cha Waigizaji lakini hadi sasa Chama chenye nasema ni sawa kama kimekufa hakuna hata mtu anayekuja katika mikutano pamoja na taarifa kuwafikia” Anaongea Mboto kwa uchungu.

Anasema kuwa lengo la kuanzisha umoja wao lilikuwa na maana nzuri kwani ilikuwa ni pamoja na kuepuka mfumo uliopo kwa Wachekeshaji kutengwa na Wayarishaji katika malipo tofauti na Wasanii wa filamu, pili kuweka mwongozo kwa kubororesha Mavazi, kupunguza mfumo wa Wachekeshaji kibao kushiriki katika Komedi moja na kushindwa kuelewa Mhusika mkuu ni nani?

Mboto pamoja na kuwa ndiye Mchekeshaji pekee anayetumika sana katika Video za Wasanii mbalimbali wa Muziki wa kizazi kipya kuigiza katika nyimbo nyingi, pia amewaonya wale wasanii wa muziki ambao umwendea bila kuwa na bajeti kwa ajili ya yeye kushiriki katika kunogesha nyimbo zao waache tabia hiyo kwani yeye anapoigiza ni sehemu yake ya kazi kwa hiyo lazima alipwe, Mboto anamba sokoni na Komedi Nampenda Mke wangu.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.