Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
22 Julai 2011

Msama Tupo Pamoja, Kanyaga Twende

Msama Tupo Pamoja, Kanyaga Twende

KAMPUNI ya ufilisi na udhamini ya Msama Promotions imeonyesha njia ya kuwasaidia wasanii kwa kuanza kukamata kazi mbalimbali za wasanii katika maeneo tofauti.

Hatua ya Msama kuanza msako wa kukamata wezi wa kazi za wasanii imetokana na kukithiri kwa wizi wa kazi ambazo ni jasho la wasanii waliojipanga kimaendeleo kupitia sanaa.

Msama amejitoa mhanga kufuatia kufanya kazi ambayo imewashinda vigogo waliopita katika nyandhifa mbalimbali za serikali ambao wanaonekana kupuuza utekelezaji wa sheria za hakimiliki na shiriki.

Kwa kuwa Msama ameanzisha utaratibu huo wa kusaka wezi wa kazi za sanaa, hapana budi wadau wengine kujitokeza kwa wingi ili kukomesha na kuondoa kabisa tatizo hilo ambalo linawarudisha nyuma wasanii.

Katika utekelezaji wake inatakiwa kishirikishwe kwa karibu Chama cha Haki Miliki na Shiriki Tanzania (COSATA) ili zoezi liende kwa mtindo ambao utafanikisha mwenendo huo kwa sababu wao ndio watendaji wakuu wa masuala hayo.

Kwa sasa COSOTA inajipanga na marekebisho ya sheria za Hakimiliki na Shiriki ambayo inafanyiwa kazi na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Achilia mbali mabadiliko hayo pia wadau wengine wa sanaa waonyeshe nia ya kukomesha njia hiyo kwa kupambana ipasavyo na masuala hayo kuliko kuketi pembeni na kumuachia Msama peke yake.

Kwa kuwa Msama ameshayavulia maji nguo, hana budi kuyaoga na si kuishia njiani jambo ambalo litazidi kuwakatisha tamaa wasanii ambao kwa sasa wanajihesabu wamepata mtetezi.

Hadi hapa ilipofikia, usipatikane upinzani kutoka kwa watendaji kutoka serikalini watakaowakingia kifua baadhi ya ndugu zao watakaopatikana na hatia ya wizi wa kazi za wasanii.

Tanzania Daima ni taasisi ambayo iko karibu na wasanii hapa nchini, imejipanga kushirikiana na wadau hao walioanzisha utaratibu wa kusaka wanaoiba kazi za wasanii Tanzania.

Hivi karibuni taasisi ya Fleva Unit nayo imejitokeza na kutangaza kupambana na maharamia wa kazi za wasanii ikiwa ni moja ya nguvu ya kukomesha wezi hao.

Nyanja ya sanaa ikifanyiwa kazi ipasavyo na wadau kudhibiti wizi, ina uwezo wa kuiingizia serikali pato kubwa zaidi ya inavyodhaniwa na wachache wenye uroho wa kula vyakula wasivyovitolea jasho.

Wasanii ongezeni nguvu baada ya kupata mwanzo kutoka kwa Msama.

Msaada zaidi wa kufanikisha udhibiti wa wizi wa kazi za wasanii, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, iongeze kasi ya kupitia mapendekezo ya Hakimili na Shiriki ili yapelekwe kwenye mjadala bungeni.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.