Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
22 Julai 2011

Wachekeshaji Wanavyoibeba Bongo Flava

Wachekeshaji Wanavyoibeba Bongo Flava

KARIBUNI wapenzi wa safu hii ya vunjavunja inayokupatia nafasi ya kutambua mambo yanayoendelea katika tasnia ya filamu za hapa nyumbani.

Mada itakayokuwa mbele yetu nitajaribu kuzungumzia kundi la waigizaji wa filamu au michezo ya uchekeshaji wa hapa nyumbani.

Pamoja na kwamba kundi hili limekuwa likidharauliwa na watu wa kada mbalimbali ikiwamo hata kwa wasanii wenzao ambao ambao hawachezi vichekesho.

Ukianzia katika maisha ya kawaida kundi hilo limekuwa likichukuliwa kama watu wa kawaida kwa vijana wa sasa wanasema ‘kuwachukulia poa’.

Kiasi cha kufikia kulalamikia kupunjwa malipo yao ambayo hulipwa ‘pesa mbuzi’ zisizoendana na kazi halisi wanazokuwa wanazifanya katika filamu wanazokuwa wanashikilishwa ukilinganisha na wale ambao wanaigiza katika sehemu za kawaida.

Kundi hilo limekuwa likijikuta hata linapokwenda kuuza kazi zake kwa kuwasambazaji maarufu kama Wadosi wamekuwa wakiwaminya kwa kuwalipa kiasi cha chini cha fedha tofauti na filamu nyingine za kawaida bla kujali kuwa wanapoziingiza sokoni huziuza kwa bei ile ile kama ya zile za kawaida.

Kazi zao zimekuwa na soko kubwa kutokana na kuwa na mashabiki lukuki hali inachangia kugombewa kama njugu.

Pamoja na hayo yote lakini wasanii hawa hivi sasa wameendelea kuonekana kuwa lulu hali inaoonyesha hakuna jambo la sanaa kupendeza pasipo kuwashirikisha wasanii hawa.

Sanaa ambazo ninazimaanisha hapa ni zile za muziki wa hapa nyumbani ikiwamo zile za kizazi kipya, filamu, matangazo na nyinginezo.

Kwa leo ningependa kuzungumzia kuhusu wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakiwatumia katika video za nyimbo zao.

Katika video za nyimbo hizo wasanii hawa hawatumiki katika kuimba bali wamekuwa wakitumika katika kuigiza matukio ambayo yamekuwa yakielezea madhui ya wimbo husika.

Mmoja wa wasanii waliofanikiwa kwa mwaka huu kuonekana zaidi katika video hizo ni Mboto ambaye ameonekana katika filamu nyingi na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki kutokana na namna ya uigizaji wake.

Uwezo wa mboto umeonekana na kuwa kivutio katika video ya Hussein Machozi inayokwenda kwa jina la ‘Utaipenda’, wimbo wa Sajna wa ‘Sitaki kuumizwa’ na nyingine.

Sharomilionea ni msanii mwingine anaye kuja juu kwa sasa na kujichukulia sifa kemkem katika kushirikishwa kwenye filamu hizo ukiachilia ile video yake ya ‘Milionea’, Lofa iliyoimbwa na Top C, Mizimu wa Hussein Machozi.

Wengine wanaokuwa wanaonekana katika video za waimbaji wa bongo fleva ni Masele ‘Chapombe’, mkono, Bambo, Erick, Kingwendu, Malingo saba mara sabini na wengine wengi.

Na Shaaban Matutu

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.