Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
22 Julai 2011

Wasanii, Hima Tuwasambaratishe Wezi Wetu

Wasanii, Hima Tuwasambaratishe Wezi Wetu

AHLAN wasahlan msomaji wa safu ya Busati inayokufikia kila siku kama ya leo kila wiki.

Ama baada ya salamu, mimi sijambo na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwa na wewe tena siku ya leo.

Msomaji wangu leo nimekuja na wazo binafsi, hasa linalohusu masilahi ya wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Bongo Flava, ambao hivi sasa wameshtuka na kuamua kuungana katika kudai haki zao za muziki, ambazo wamekuwa wakidhulumiwa na kuibiwa kwa takriban muongo mmoja sasa.

Ndiyo wasanii wa Bongo Flava wamezinduka kwa hilo, binafsi nawapa kiganja bila wasiwasi, kwani wanastahili, ila jambo muhimu kwao ni kuwa na mshikamano na umoja wenye nguvu.

Ni kweli umoja pekee ndiyo utakaowawezesha kuwaweka huru na kufurahia matunda ya kazi zao endapo watafanikiwa kuziba mianya ya wezi waliokubuhu kwa kuwanyonya wanamuziki hawa ambao muziki umekuwa ndiyo sehemu ya ajira yao.

Wasanii wa muziki huo wameasisi Chama cha Flava Unit, wakiwa chini ya Mwenyekiti wao, Hamis Mwinjuma, maarufu kwa jina la MwanaFa, ambaye pia ni msemaji mkuu wa chama hicho kilichoundwa na wasanii wenye amafanikio na wale wachanga huku wakiwa wamejipanga kupeleka muswada wao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kuidai serikali iunde sheria ya kulinda kazi za wasanii wa muziki hapa nchini na kuwapa rungu la kuwakamata wezi wote wa kazi zao.

Jambo la muhimu kwa wasanii hawa ambao wameshtukia wizi huu wawe kitu kimoja ndiyo nguzo kubwa na msingi wa wao utakaowaweka huru na kuwawezesha kupata haki yao.

Nasema hivyo kwa sababu wasanii wengi wamekuwa na hulka ya kupenda sifa na ukubwa, hivyo hata wakisikika wameungana, mwisho wa siku na kabla ya kufikia lengo, husambaratika na kuwasikia wakiwa wamejitenga wenye uzoefu na majina na wale wachanga.

Hapa ndipo tunapong’amua kwamba wasanii waliokuwa kwenye gemu muda mrefu huwa wanajisahau walikotoka na wakati mwingine ni ulimbukeni tu wa fani, kwani siku zote mtu akisota sana na mara anapopata hujikuta akiwadharau wengine kuliko ninavyoweza kuelezea. Majina na mifano ipo, ila kwa leo nawapotezea tu.

Mwenyekiti wa chama hicho, MwanaFa, anazungumza kwa niaba ya wasanii na wanachama wa Chama cha Flava Unit kwamba wamejipanga kwa lengo la kupigania haki zao za msingi za muziki. Mimi nawaambia inshaallah, ikiwa mmeweka nia kila kitu kitakuwa sawa.

Aidha, wasanii hao pia wamejipanga kwenda Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA), ambako wanataka kulipa kodi ili waweze kupata stika ikiwa ni njia moja ya kudhibiti wizi wa kazi za wasanii.

Ni jambo la kusikitisha sana, hasa pale tunapoona msanii akiwa ameachia ngoma yake studio tu lakini wezi tayari wanakuwa na wimbo huo barabarani kama si mtaani, huku kukiwa hakuna jinsi ya kuweza kumkamata.

Hadi sasa faini kwa mtu yeyote anayeiba kazi ni sh 50,000, ambayo wasanii wamekuwa wakilia, kwa sababu haisaidii, kwani hata mtu akikamatwa ana uwezo wa kulipa. Mtuhumiwa anatengeneza fedha nyingi zaidi ya hiyo. Naomba sheria hii ibadilishwe, kwani ni ya muda mrefu - tangu enzi za Mwalimu Nyerere, ikibadilishwa ninaamini ndipo wasanii watapata haki zao.

Na Khadija Khalili

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.