Jina la Usajili:  Neno la Siri:    Umesahau neno la siri?   |   Umesahau jina?
25 Julai 2011

Soko Limefurika, Filamu Inazama - Kambi

Soko Limefurika, Filamu Inazama - Kambi

MSANII Muigizaji mahiri wa filamu kutoka Tanzania Hashim Kambi amelalamikia utoaji wa filamu kwa fujo ambao yeye ameuita kama ni utitiri wa Filamu, kuwa ni sehemu ya kifo cha wasanii waigizaji pengine hata wadau wanaohusika na tasnia hii kwa ujumla, akiongea na FC katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, amesema kuwa binafsi hakubaliani na mfuom unaotumika katika kuingiza filamu sokoni.

“Kwa sasa ni sawa na fujo kwani filamu ni nyinyi sana wakati nikiangalia kuwa soko ni lile halina mabadiriko, lakini jambo lingine ni kuwa kutokana na utoaji wa filamu kila mara tena kwa wingi bila kuzingatia wanunuzi kuhusu mahitaji yao kuwa wanaweza kununua kazi zetu kwa spidi hivyo hilo nalo ni tatizo lingine hali ya sasa si shwari kwa wasanii na wadau wote kwa ujumla” Anasema Ramsey

Aidha amesema kuwa anajua kuwa watu wengi wanajiuliza kuwa kwanini wao wamekuwa wakishiriki katika filamu nyinyi kwa wakati mmoja bila kutoa muda kwa wapenzi wao, lakini jibu lake ni kwamba kutokana na wingi wa filamu anajikuta kuwa hana jinsi kwani malipo ya filamu hizi yamekuwa ni madogo kwa mantiki hiyo ili maisha yaendelee inamradhimu msanii kuigiza filamu nyingi kadri awezavyo ili mradi apate Riziki.

Ramsey ni mmoja kati ya wasanii wanaongoza kwa kuigiza filamu nyingi nchini Tanzania akiwa sambamba na wasanii kama vile Charles Magari (Mzee Magari) Ahmed Olotu (Mzee Chilo) na wasanii wengine.

Login to post comments

MSANII WA WIKI

Loveness

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa Filamu Tanzania Loveness Watson Nyota yake kwa sasa inatingisha katika tasnia ya

Soma Zaidi...

VIDEO YA MHARIRI

Off Side

Si mara ya kwanza kutazama filamu za Kanumba, lakini pia ni ukweli kwamba kila filamu anayokuja nayo

Soma Zaidi...

FILAMU ZA BONGO

Mbawa za Dino Zafunguka

MUIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu hapa nchini Tanzania Dennis Sweya (Dino) anatarajia kuanza kurekodi

Soma Zaidi...

WAHAPAHAPA VIDEO

You need Flash player 6+ and JavaScript enabled to view this video.