25 Julai 2011

Baby Madaha Ahitimisha "Tifu la Mwaka"

Baby Madaha Ahitimisha "Tifu la Mwaka"

MWANAMUZIKI na Muigizajia mahiri katika tasnia ya filamu Baby Madaha amemaliza kurekodi filamu ya Tifu la Mwaka, ikiongozwa na Gwiji la Filamu na Muongozaji wa filamu Issa Mussa aka (Cloud 112) akiongea na FC Baby ameieleza FC kuwa katika filamu hii amekamua ile mbaya na anaamini kila mtu ambaye atabahatika kuoiona filamu hii atakubaliana na maneno yake.

“Nimalizia kazi yangu ya kurekodi filamu ya Tifu la Mwaka, hivi sasa nipo katika hatua za mwisho kushughulikia wimbo wangu mpya ambao natarajia kuutoa mwishoni mwa mwezi wa August, baada ya kucheza filamu yangu ya Ray of Hope ndio nimerudi tena kwa nguvu katika kuigiza filamu hii ya Tifu la Mwaka ya Cloud, ni filamu nzuri ndiyo maana nimekubali kuigiza” Aliiambia FC Baby.

Baby Madaha ndiye msanii pekee kwa sasa ambaye ameweza kumudu kuwa katika fani mbili kwa wakati mmoja,yaani filamu na Muziki lakini wasanii wengi udumu katika fani moja tu, tayari nyota huyu ameshiriki filamu kama vile House No. 44, Misukosuko, Desperando, Ray of Hope na filamu nyingine, filamu ya Tifu la Mwaka imewashirikisha wasanii kama Barafu Seleiman, Ummy Wenslaus (Dokii), Issa Mussa (Cloud112) Baby Madaha na wasanii wengine.